GET /api/v0.1/hansard/entries/426232/?format=api
HTTP 200 OK
Allow: GET, PUT, PATCH, DELETE, HEAD, OPTIONS
Content-Type: application/json
Vary: Accept
{
"id": 426232,
"url": "https://info.mzalendo.com/api/v0.1/hansard/entries/426232/?format=api",
"text_counter": 180,
"type": "speech",
"speaker_name": "Sen. Chelule",
"speaker_title": "",
"speaker": {
"id": 13126,
"legal_name": "Liza Chelule",
"slug": "liza-chelule"
},
"content": "Asante sana, Bwana Spika wa Muda. Nimesimama kuunga mkono Hoja hii ambayo imeletwa na Sen. Karaba. Ningependa kuchukua nafasi hii kumpongeza. Nina sababu tatu za kuunga mkono Hoja hii ya masomo ya watu wazima. Tunaelewa kwamba kuna watu ambao hawakubahatika katika jamii kusoma kwa sababu ya ukosefu wa pesa na mambo mengine kama vile wazazi kutengana. Wengine ni wasichana ambao walipata mimba wakiwa shule na wakalazimika kuwacha masomo. Ninasema hivi kwa sababu kuna akina mama wengi ambao hawakubahatika katika masomo. Tungependa kuiinua nchi yetu na uchumi wetu. Tumekuwa tukiongea na watu wetu kuhusu mambo ya kilimo. Itakuwa maajabu akina mama wakitaka kufanya biashara lakini hawajui kupima mbolea na vile watakavyofanya mambo mengine. Kuna pesa ambazo Serikali imewatengea wanawake na vijana. Wanawake huwa na shida sana ya kuandika kumbukumbu za mikutano na kufanya mipango ya biashara. Wanawake pia huwa na shida ya kujua vile watakavyotumia pesa zao. Wao huzunguka vijiji wakiwatafuta wale ambao wamesoma. Kwa hivyo, Hoja hii ni ya maana sana. Lazima tuwe na kamati ambayo itayasimamia masomo ya watu wazima na vile tunavyoweza kupata waalimu wa kuwashughulikia. Sote tunajua kwamba Serikali ilikuwa na mpango huo wa elimu ya watu wazima lakini, hatujui ni kwa nini haijakuwa ikifanya kazi vile inatakikana. Hoja ya Sen. Karaba itatusaidia kama nchi na akina mama. Leo tunaongea kuhusu kuwaelimisha watu kuhusu Katiba. Katiba ni chombo cha maana katika nchi yetu. Hiki ni chombo ambacho ni lazima kila mtu ajue ni nini imeandikwa katika Katiba hii. Kwa hivyo, itakuwa vizuri sana tukiwa na masomo hayo ya watu wazima kwa sababu kina mama watakuwa na nafasi ya kusoma. Vile vile, watakuwa na nafasi ya kusoma hii Katiba ili waelewe vizuri kuna nini ndani ambayo inawahusu. Tena, Bw. Spika wa Muda, masomo haya yatawasaidia kina mama na watu wote katika kusoma Bibilia. Nasema kina mama kwa sababu hawa ndio wanaotaabika na shida nyingi sana. Kukiwa na shida katika jamii – kwa mfano mama na baba wametengana – The electronic version of the Senate Hansard Report is for information purposes only. A certified version of this Report can be obtained from the Hansard Editor, Senate."
}