GET /api/v0.1/hansard/entries/426234/?format=api
HTTP 200 OK
Allow: GET, PUT, PATCH, DELETE, HEAD, OPTIONS
Content-Type: application/json
Vary: Accept
{
"id": 426234,
"url": "https://info.mzalendo.com/api/v0.1/hansard/entries/426234/?format=api",
"text_counter": 182,
"type": "other",
"speaker_name": "",
"speaker_title": "",
"speaker": null,
"content": "yule mtu anayeumia sana ni msichana. Kwa hivyo, wengi wao waliwacha shule kwa sababu ya shida mbali mbali wakati ambao hawangefaa kuwacha shule. Ndio maana unasikia nikisema mara nyingi ni kina mama. Kwa hivyo, naunga Hoja hii ya Sen. Karaba mkono kwa dhati nikiwa mmoja wao; niko nyuma yao. Bw. Spika wa Muda, kuna masomo ambayo sisi sote tunatakikana kuendelea kusoma. Sisemi kuwa Hoja hii iwe inahusu wale watu ambao hawakuenda shule peke yao; kwa sababu ya teknolojia mpya, sisi sote tunatakikana kuendelea kusoma. Kwa hivyo, naunga mkono nikisema kwamba ikianzishwa, isimamiwe kwa njia bora; ihakikishwe kwamba ni masomo ambayo ni updated, ama ni masomo ya kisasa; masomo ambayo wataweza kusoma mambo ya tarakilishi na mengine kwa sababu mambo yanabadilika kila mara. Kwa hivyo, Bw. Spika wa Muda, naunga mkono Hoja hii ya Sen. Karaba."
}