GET /api/v0.1/hansard/entries/426286/?format=api
HTTP 200 OK
Allow: GET, PUT, PATCH, DELETE, HEAD, OPTIONS
Content-Type: application/json
Vary: Accept
{
"id": 426286,
"url": "https://info.mzalendo.com/api/v0.1/hansard/entries/426286/?format=api",
"text_counter": 234,
"type": "speech",
"speaker_name": "Sen. (Dr.) Zani",
"speaker_title": "",
"speaker": {
"id": 13119,
"legal_name": "Agnes Zani",
"slug": "agnes-zani"
},
"content": "Asante, Bwana Spika wa Muda, kwa nafasi hii ya kuunga mkono Hoja hii ambayo ni muhimu sana. Hoja hii, ambayo tumekuwa tukiizungunzia, ni ya kuumiza roho. Haya ni mambo ambayo tumekuwa tukizungumzia kwa muda mrefu. Asante, Sen. Omar, kwa kuleta Hoja hii. Tulingojea hadi watu wakaumizwa wakiwa kanisani ili tukawa na Hoja hii. Katika nchi hii, tutafika wakati ambapo tutaogopa kulala usiku kwa sababu hatutaweza kujua hatari ambazo zinaweza kutokea. Watu watano ambao wameuwawa na wale kumi na saba ambao walipata majeraha hawakujua kama mambo hayo yangetokea. Walienda kule kumwabudu Mungu. Naona kutafika wakati ambapo watu wataogopa kwenda kanisani. Watu wataanza kusikiza burudani wakiwa nyumbani kwa sababu ya hofu. Tukio hilo la Joy in Jesus Church lilituweka katika hali ya mshangao. Hili ni jambo ambalo pia limeshangaza Gavana wa Kaunti ya Mombasa. Gavana wa Mombasa amejaribu sana kwa kuweka magari ya metropolitan police, kwa kimombo, kuhakikisha usalama lakini unga umezidi maji. Mambo ya usalama yamekuwa magumu zaidi. The electronic version of the Senate Hansard Report is for information purposes only. A certified version of this Report can be obtained from the Hansard Editor, Senate."
}