GET /api/v0.1/hansard/entries/426288/?format=api
HTTP 200 OK
Allow: GET, PUT, PATCH, DELETE, HEAD, OPTIONS
Content-Type: application/json
Vary: Accept
{
"id": 426288,
"url": "https://info.mzalendo.com/api/v0.1/hansard/entries/426288/?format=api",
"text_counter": 236,
"type": "other",
"speaker_name": "",
"speaker_title": "",
"speaker": null,
"content": "Ni vizuri kwamba tuna viongozi wengi ambao wamejitokeza hasa kutoka dini ya kiislamu kukashifu jambo hili. Kama mambo hayangefanyika hivyo, haya yangeonekana kama mapigano baina ya Wakristo na Waislamu. Mambo hayo hayatakiwi kuendelea. Tumeelezwa, kupitia vyombo vya habari kwamba siku hiyo, walitaka kwenda kwa kanisa lingine kuuwa watu wengine. Lakini kwa bahati nzuri, walipofika pale, askari aliyekuwa mlangoni akakuwa amejihami. Kwa hivyo, ikawa vigumu kwao kuingia pale. Walipoona akiwa na risasi ikawa vigumu kwao kuingia pale. Kwa hivyo, ni kama walikuwa wamejipanga kwenda mahali tofauti. Kabla hatujapumzika kutoka kisa cha Msikiti wa Majid Musa, kulikuwa na warsha. Katika warsha hiyo, watu walikuwa wakielezwa mambo ya dini na kukatokea vurugu. Vurugu hiyo ilianzishwa na viongozi ambao wanaangalia mambo ya usalama. Watu hao waliingiliwa na kufukuzwa hadi watoto wakaumia. Ilibidi wengi wapelekwe jela na mashtaka yao bado hayajakamilika. Kidonda hicho kilikuwa bado cha tuliza na vidonda vingine bado vya tuliza. Si muda mfupi baada ya hapo, Sheikh Ali Bahero aliingiliwa mchana na wala si usiku akiwa anaendelea na mafundisho. Vijana wake ambao pengine hawakukubaliana na vile alivyokuwa akizungumza walimuingilia. Usalama uko wapi? Tunajiuliza, Serikali kuu iko wapi mambo haya yakiendelea? Mambo ya usalama yakiendelea kuzoroteka tutafika wakati ambapo itakuwa vigumu kwa mtu yeyote kuwa na usalama mahali popote. Kabla hatujapumzika, juzi juzi tena, katika Kaunti ya Mombasa, vilipuzi vilipatikana. Grinedi hizi ziliingia humu nchini vipi? Walinda usalama walikuwa wapi? Kama walipitia katika uwanja wa ndege, walipita vipi? Haya ni maswali ambayo tunajiuliza kila wakati. Ni nani ambao walihusika na kwa nini hawapatikani? Ni kisa gani ambacho walitaka kufanya? Hatuwezi kuyasahau mambo yaliyofanyika Westgate ambapo watu waliumia na wengine wakafariki. Kwa hivyo, hali hii ya kuogopa imeikumba nchi hii na inawafanya watu waendelee kuogopa kila siku. Mombasa ni mji wa kitalii. Watu wanatembea Mombasa na Malindi kwa sababu ya utalii. Watalii ni watu ambao wanaogopa sana mambo ya usalama. Wao huwa wanauweka usalama wao mbele. Wakifika mahali ambapo wanaogopa wakiona usalama wao hauko sawa, wao hutoweka. Juzi, nikiwa Mombasa katika hoteli, nilipata kwamba hoteli hazina watu. Juzi, nikiwa Kwale County, pia nilitembelea hoteli, nilipata hakuna watu. Watu wamefutwa kazi kwa sababu hakuna biashara. Kisa na maana ni usalama. Hili ni jambo ambalo tunaweza kuliangalia na kuhakikisha tumelisimamisha na kulitatua. Hatuwezi kuwa tukizungumza tu. Serikali kuu iko wapi mambo haya yakiendelea? Vijana wetu wanafaa kupata kazi na kuendelea kulinda usalama."
}