GET /api/v0.1/hansard/entries/426292/?format=api
HTTP 200 OK
Allow: GET, PUT, PATCH, DELETE, HEAD, OPTIONS
Content-Type: application/json
Vary: Accept
{
"id": 426292,
"url": "https://info.mzalendo.com/api/v0.1/hansard/entries/426292/?format=api",
"text_counter": 240,
"type": "speech",
"speaker_name": "Sen. Boy Juma Boy",
"speaker_title": "",
"speaker": {
"id": 758,
"legal_name": "Boy Juma Boy",
"slug": "boy-juma-boy"
},
"content": "Asante sana, Bwana Spika wa Muda, kwa kunipa nafasi hii. Kwanza, ningependa kutoa rambi rambi zangu kwa familia ambazo ziliathiiriwa na mkasa wa Likoni. Ningependa kuungana na wenzangu kutoa rambi rambi kwa majirani wangu wa Mombasa ambao waliwapoteza jamaa wao. Kama mnavyojua, natoka Kwale na sisi ni majirani wa watu wa Mombasa, sawa tu na pua na mdomo. Kitendo kilichotendeka Likoni hakikubaliki katika Kenya ya sasa. Hakikubaliki! Ningependa kuieleza Seneti hii kwamba hilo si la Kiislamu. Hili ni jambo la watu wachache walio na mawazo machafu; mawazo ambayo hayakubaliki; mawazo ambayo katika lugha twaweza kusema ni tasa, ambayo hayazalishi. Ukweli wa mambo ni kwamba mtu aliye na fikira za kwenda kuua katika kanisa watu walioenda kuabudu, ni mtu aliye na fikira mbaya. Mimi kama Seneta ningependa kuiomba Serikali kuhakikisha National Intelligence Service (NIS) inafanya kazi nzuri ya kugundua mabomu yalitoka wapi Mombasa. Tunafaa kusaidiwa kupata fedha za ziada ili tufanye uchunguzi. Maoni yangu ni kuwa kikosi cha polisi kipewe fedha nyingi ili kiweze kufanya uchunguzi na upelelezi The electronic version of the Senate Hansard Report is for information purposes only. A certified version of this Report can be obtained from the Hansard Editor, Senate."
}