GET /api/v0.1/hansard/entries/426294/?format=api
HTTP 200 OK
Allow: GET, PUT, PATCH, DELETE, HEAD, OPTIONS
Content-Type: application/json
Vary: Accept

{
    "id": 426294,
    "url": "https://info.mzalendo.com/api/v0.1/hansard/entries/426294/?format=api",
    "text_counter": 242,
    "type": "other",
    "speaker_name": "",
    "speaker_title": "",
    "speaker": null,
    "content": "zaidi juu ya suala hili. Swali ni; silaha zilizotumika zilitoka wapi? Ni lazima tujue hawa watu walitoa wapi bunduki za AK47 zilizotumika kuwauwa watu wasiokuwa na hatia. Hilo ni jambo ambalo halikubaliki katika Kenya yetu ya leo. Sisi kama viongozi wa Kenya bila kujali dini zetu, ni lazima tulaani kitendo hiki cha ugaidi. Hiki ni kitendo kilichotendwa na waoga. Je, wahalifu hawa hajui kambi yetu ya wanajeshi ilipo? Watu fulani wanadai kitendo hiki kimefanywa kwa sababu Kenya Defense Forces (KDF) wako nchini Somalia. Kwa nini mtu awe na mawazo chafu ya kuwauwa watu ambao hawana hatia? Hili ni jambo ambalo linahitaji kulaaniwa na viongozi wote wa dini, wakiwemo wa Kikristo, Kiislamu, Kihindi na wa dini zote hapa nchini. Hili ni jambo ambalo halikubaliki hapa. Bw. Spika wa Muda, juzi Sen. Hassan aliomba taarifa kuhusu swala la mauaji ya viongozi wa kidini kule Mombasa. Taarifa hiyo haijawahi kuletwa mbele ya Seneti hii. Jambo hili la usalama limechukuliwa kimchezo. Ninakumbuka Bw. Spika ukiamrisha taarifa hiyo iletwa hapa wiki hii. Kabla taarifa hiyo kuletwa hapa, janga lingine linakumba taifa letu. Utovu wa usalama umeenea sana nchini. Hali hii yakutia hofu ni moja kati ya mbinu ambazo tusipozichunguza kwa makini, zitahakikisha kwamba twaenda mahali pabaya. Ikiwa hatutatumia busara katika jambo hili tunaweza kugonganishwa wenyewe kwa wenyewe. Hili ni jambo ambalo haliko katika mawazo ya wengi wetu. Sisi kule kwetu tunaishi na watu wa kila aina. Tunafanya michango kanisani na misikitini. Sisi hushirikiana sote. Ni vigumu kumtambua Muislamu na Mkristo kwa sababu tunaishi pamoja na kwa amani. Sisi sote twaishi kama Wakenya na kama watu wa kabila moja. Lakini lazima mzizi huu wa utovu wa usalama utafutwe kabla haujaenea zaidi. Kuna daktari mmoja anayeitwa pathologist . Yeye haoni mgonjwa lakini huona maiti. Kazi ya pathologist ni kuuliza “amekufaje?” Daktari ni daktari; haoni mtu mzima, ukipelekwa kwa pathologist, basi ujue ushakufa; you are dead! Kazi ya pathologist ni kutafuta chanzo cha kifo. Hujaribu kujibu kilichosababisha kifo. Sasa isiwe kazi yetu sisi kufanya kazi ya daktari huyu ambaye hujishughulisha na kilichosababisha kifo. Sisi tunahitaji daktari wa kutibu, si wakujua kilichosababisha kifo."
}