GET /api/v0.1/hansard/entries/426300/?format=api
HTTP 200 OK
Allow: GET, PUT, PATCH, DELETE, HEAD, OPTIONS
Content-Type: application/json
Vary: Accept
{
"id": 426300,
"url": "https://info.mzalendo.com/api/v0.1/hansard/entries/426300/?format=api",
"text_counter": 248,
"type": "other",
"speaker_name": "",
"speaker_title": "",
"speaker": null,
"content": "ninatoka Kaunti ya Kilifi. Napeana pole kwa familia za wale ambao walipoteza maisha yao. Pia nawaombea wale waliojeruhiwa wapate afueni ya haraka. Pia nawaombea wote wale ambao walikuwa katika lile Kanisa Mwenyezi Mungu awape nguvu kwa sababu hicho kitendo ni cha kutisha. Pia wale ambao wamefiwa na jamaa zao, nawaomba pia wawe na subira kwa sababu Serikali yetu lazima itachunguza ilikuaje na ilikwendaje. Bw. Spika wa Muda, hili suala la usalama ni letu sisi sote. Tusije kulaumiana. Ikija wakati kama huu, kila mtu awaajibike kwa sababu hawa watu waliotekeleza uovu huu ni watoto wetu, ni ndugu zetu na jamaa zetu. Utakuta kwamba ni watu wanaojulikana, lakini hakuna mtu ambaye atajitokeza kusema ilikuwa vipi na ilikwenda vipi. Lazima Wakenya wote wachukue jukumu; lazima tuwe na macho wazi na tusikubali hata kamwe kuharibiwa nchi na watu wachache ambao wako hapa ili kusema Kenya haina usalama wa kutosha. Bw. Spika wa Muda, ukiangalia hata wale waliokwenda Masjid Musa, utakuta ni vijana wetu. Utakuta ni watu wetu tunaowajua. Ikiwa mtu amebeba silaha, ni lazima mtu mwingine alimuona. Wakati mwingine mtu huyo walipanga kutekeleza kitendo hicho na watu wengine. Bw. Spika wa Muda, ni huzuni kubwa kwa sababu kama unafanya kazi hotelini, hoteli hiyo inawanufaisha watu wengi. Hoteli inamnufaisha hata muuza mboga au mtu ambaye anatumia matatu kwenda kazini au mahali popote. Sasa iwapo hizi hoteli zetu zitafungwa kwa sababu hakuna amani na usalama wetu haupo, basi Wapwani tutakula nini? Kwa sababu unaona ya kwamba Mombasa ikipigwa ama kukiwa na vurugu yoyote, Pwani nzima huwa yalala njaa. Wafanyakazi wa Pwani nzima yawabidi wakae nyumbani na hoteli zote Pwani nzima zinafungwa. Sisi katika Pwani hutegemea hotel industry . Ikiwa wageni wataogopa kuja, basi itakuwa vigumu sana kujikimu katika maisha yetu kama Wapwani. Bw. Spika wa Muda, hiki ni kitendo cha kusikitisha sana kwa sababu hata kama kitendo hiki kimefanywa na vijana wetu, wajua hauwezi kunyea mkono ambao unakulia. Hawa vijana waliotekeleza mambo kama haya wanasahau kuwa tunahitaji watalii ili tupate riziki zetu. Bw. Spika wa Muda, kwa hayo machache ninaunga mkono Hoja hii."
}