GET /api/v0.1/hansard/entries/427665/?format=api
HTTP 200 OK
Allow: GET, PUT, PATCH, DELETE, HEAD, OPTIONS
Content-Type: application/json
Vary: Accept
{
"id": 427665,
"url": "https://info.mzalendo.com/api/v0.1/hansard/entries/427665/?format=api",
"text_counter": 378,
"type": "speech",
"speaker_name": "Sen. Mwakulegwa",
"speaker_title": "",
"speaker": {
"id": 101,
"legal_name": "Danson Mwazo Mwakulegwa",
"slug": "danson-mwazo"
},
"content": "Asante, nimekubali ndugu yangu mkubwa kwa umri na Seneta Mwenzangu wa heshima. Ninaongea juu wa Wasomali walioko Somalia sio Wasomali walio Kenya. Wasomali ambao wako Kenya ni ndugu zetu na wao wanaishi kwa amani. Lakini kuna wale wengine ambao wamepita mipaka yetu na wakajipata Nairobi ndio sababu kumekuwa na mushkin wa amani. Ningependa kusema kwamba sisi tunapeleka majeshi yetu kule na nchi yetu itatumia hela nyingi. Kuna umuhimu wa kuona ya kwamba amani imedumishwa katika nchi za Jumuia ya Afrika Mashariki. Singependelea kuendelea zaidi lakini ni kurudi nyuma na kumshukuru Rais kwa kuchukua nafasi kuzingatia Katiba na pia kwa Mkuu wa Walio Wengi katika Bunge letu la Seneti kuleta Hoja hii. Naunga mkono."
}