GET /api/v0.1/hansard/entries/42793/?format=api
HTTP 200 OK
Allow: GET, PUT, PATCH, DELETE, HEAD, OPTIONS
Content-Type: application/json
Vary: Accept

{
    "id": 42793,
    "url": "https://info.mzalendo.com/api/v0.1/hansard/entries/42793/?format=api",
    "text_counter": 426,
    "type": "speech",
    "speaker_name": "Dr. Shaban",
    "speaker_title": "The Minister for Gender, Children and Social Development",
    "speaker": {
        "id": 139,
        "legal_name": "Naomi Namsi Shaban",
        "slug": "naomi-shaban"
    },
    "content": " Asante sana, Bi Naibu Spika wa Muda na pia Waziri wa Haki, Uwiano wa Kitaifa na Maswala ya Kikatiba kwa kunipa nafasi ili nichangie Hoja hii. Siku ya leo ni muhimu sana katika historia ya nchi hii. Waziri amewasilisha Mswada ambao utafanya nchi hii kuwa na Mahakama Kuu zaidi. Wakenya wengi wameteseka sana kwa muda mrefu, hasa wale ambao mali na mashamba yao yamenadiwa kwa sababu ya madeni. Hawakuwa na pahali pa kupeleka kilio chao. Sheria zetu zimekuwa zikiwalinda matajiri. Maskini wamekuwa wakinyimwa haki yao. Lakini tukipitisha Mswada huu, basi maskini watakuwa na pahali pa kupeleka kilio chao. Ni matumaini yangu kuwa akina mama wengi wataomba kazi kuhudumia mahakama hii. Tunataka jaji wengi wanawake katika mahakama hii. Majaji watakaohudumia mahakama hii watakuwa na jukumu kubwa la kulinda uhuru wa kila mwananchi katika nchi hii. Tungependa kuona uhuru wa mahakama hii. Haki katika nchi hii imekuwa ni ya kununuliwa. Kuna baadhi ya watu ambao wamekuwa wakitumia pesa ili wapate haki na kuwapokonya wanyonge haki yao. Serikali yetu imepoteza pesa nyingi sana kwa sababu ya ufisadi katika mahakama zetu. Mahakama hii itaokolea Serikali hii pesa nyingi sana. Ushuru ambao utapatikana kutoka kwa mahakama hii utasaidia uchumi wetu kuimarika. Tena nitampongeza Waziri kwa kazi yake katika Wizara hii. Jambo hili ni muhimu sana katika nchi hii. Tukiwa na mahakama hii tutapiga hatua za kuleta haki na uwiano kwa wananchi wote. Kwa hayo machache, ninaunga mkono."
}