GET /api/v0.1/hansard/entries/429138/?format=api
HTTP 200 OK
Allow: GET, PUT, PATCH, DELETE, HEAD, OPTIONS
Content-Type: application/json
Vary: Accept
{
"id": 429138,
"url": "https://info.mzalendo.com/api/v0.1/hansard/entries/429138/?format=api",
"text_counter": 357,
"type": "speech",
"speaker_name": "Hon. Mwaura",
"speaker_title": "",
"speaker": {
"id": 13129,
"legal_name": "Isaac Maigua Mwaura",
"slug": "isaac-mwaura"
},
"content": "Mhe. Naibu Spika, ningependa kusimama kuunga mkono Mswada huu. Kwanza, ningependa kusema kwamba ukitathmini na kuangalia hii sheria na ulinganishe na ile tuliokuwa nayo mwaka jana, ni ishara kwamba kumekuwa na mabadiliko. Kumekuwa na uwiano wa mambo ambayo tunafaa kuyaafikia kama Taifa la Kenya. Inasemekana kwamba hii sheria itazungumziwa na Bunge zote mbili - Bunge la Seneti na Bunge la Kitaifa. Ukikumbuka, kulikuwa na tashwishi na watu wakakimbia kwa Mahakama Kuu ili ieleweke ni vipi ambavyo tutaweza kuangazia swala hili. Pia, tumeona wakati uliopita kwamba kumekuwa na malumbano kati ya yale maamuzi ambayo yanafanyika kutoka katika korti zetu na kuendelea kwa Taifa. Kwa hivyo, tunafurahi kwamba Mswada huu unapendekeza ya kwamba kabla ya kukimbia kortini, watu waketi chini na kuangazia maswala tata na kuyashughulikia badala ya kwenda kortini. Pia kipengele hicho kinasema hususan kwamba ikiwa kuna afisa yeyote wa umma ambaye atafanya Serikali gatuzi ipate gharama ya kwenda kortini, basi achukuliwe hatua yeye mwenyewe kama mtu binafsi. Pia ukiangalia asilimia ya hela The electronic version of the Official Hansard Report is for information purposesonly. A certified version of this Report can be obtained from the Hansard Editor."
}