GET /api/v0.1/hansard/entries/429139/?format=api
HTTP 200 OK
Allow: GET, PUT, PATCH, DELETE, HEAD, OPTIONS
Content-Type: application/json
Vary: Accept
{
"id": 429139,
"url": "https://info.mzalendo.com/api/v0.1/hansard/entries/429139/?format=api",
"text_counter": 358,
"type": "speech",
"speaker_name": "Hon. Mwaura",
"speaker_title": "",
"speaker": {
"id": 13129,
"legal_name": "Isaac Maigua Mwaura",
"slug": "isaac-mwaura"
},
"content": "ambazo zimewekwa kufikia mashinani kupitia serikali za ugatuzi, ni kweli kwamba zimeongezeka kwa kiasa cha asilimia 43. Lakini pia tumekuwa na mazungumzo kama Kamati ya Bajeti na Makadirio kwamba kulikuwa na kiwango ambacho kilikuwa kimependekezwa na ile Tume ya Ugavi wa Rasilmali cha Kshs279 bilioni. Tulitoka pale hadi Kshs238 bilioni. Kwa hivyo, huu mchakato lazima uendelee kwa sababu sijui kana kwamba kupunguza kule ni kutokana na majukumu ambayo yamezidi katika Serikali ya Kitaifa. Pia ukiangalia zaidi, nafikiri Wakenya wamekuwa na mwito wa kuhakikisha kwamba hakuna rushwa ambayo inajikidhiri katika maeneo ya mashinani kupitia mifumo ya serikali za ugatuzi. Lakini pia tujue kwamba vile ambavyo tunapiga msasa serikali za ugatuzi, ndivyo ambavyo tunatazamiwa pia kupiga msasa Serikali ya Kitaifa. Kuna mwandishi mmoja ambaye anaitwa John C. Maxwell ambaye anasema kwamba ndiposa ufaulu, ni lazima ufanye makosa. Nafikiri mwaka huu ni wa kwanza. Kwa kweli, tumeona kwamba serikali za ugatuzi zimefanya makosa na kutoka hapa kusonga mbele, kutakuwa na mwito mpya kuhakikisha kwamba wananchi wanapata huduma. Wananchi wanapata dhamana ya zile hela ambazo zinapelekwa katika serikali za ugatuzi. Ukiangalia Mswada huu, unaelezea kinaga ubaga jinsi ambavyo pesa zilizotengwa zitatumika. Jambo ambalo linanifurahisha ni kuona ya kwamba tumepatiana hela za kuboresha polytechnics katika kila kaunti ya nchi hii. Pia, kuna hela za kuboresha mahospitali."
}