GET /api/v0.1/hansard/entries/429143/?format=api
HTTP 200 OK
Allow: GET, PUT, PATCH, DELETE, HEAD, OPTIONS
Content-Type: application/json
Vary: Accept
{
"id": 429143,
"url": "https://info.mzalendo.com/api/v0.1/hansard/entries/429143/?format=api",
"text_counter": 362,
"type": "speech",
"speaker_name": "Hon. Mwaura",
"speaker_title": "",
"speaker": {
"id": 13129,
"legal_name": "Isaac Maigua Mwaura",
"slug": "isaac-mwaura"
},
"content": "Mhe.Naibu Spika, pia,ni jambo la kutajika kuona kwamba kuna hela ambazo zimetengwa za kuinua miradi ambayo inafaa kusaidia uchumi wetu uweze kukua kwa kiwango ambacho kinafaa. Jambo la kusikitisha ni kwamba Kenya inaorodheshwa kufikia mwezi wa Septemba kuwa na uchumi ambao ni wa nne bora zaidi katika ukanda wa Afrika. Lakini jambo ambalo tunafaa kuangazia ni, ni vipi tutaweza kuweka pesa mashinani ambazo zitawasaidia wananchi kupata ajira? Hii ni kwa sababu ukuaji wa uchumi pasipo na ajira si jambo ambalo linasaidia kwa sababu linafanya maskini wawe maskini zaidi na mabwenyenye waendelee kuwa mabwenyenye na matajiri zaidi. Kwa hivyo, ni jambo ambalo tunafaa kuangazia ili tuweke masharti ya utumizi wa pesa kuhakikisha kwamba hela ambazo zinafika mashinani zinasaidia kuleta ajira na kuinua kiwango cha uchumi hususani katika familia."
}