GET /api/v0.1/hansard/entries/429146/?format=api
HTTP 200 OK
Allow: GET, PUT, PATCH, DELETE, HEAD, OPTIONS
Content-Type: application/json
Vary: Accept

{
    "id": 429146,
    "url": "https://info.mzalendo.com/api/v0.1/hansard/entries/429146/?format=api",
    "text_counter": 365,
    "type": "speech",
    "speaker_name": "Hon. Mwaura",
    "speaker_title": "",
    "speaker": {
        "id": 13129,
        "legal_name": "Isaac Maigua Mwaura",
        "slug": "isaac-mwaura"
    },
    "content": "Mhe. Naibu Spika, pia ningependa kusema kwamba ni muhimu katika hiyo miradi kuhakikisha ya kwamba asilimia ya watu walemavu ambao wanaishi mashinani ni 79. Kwa hivyo, ni muhimu katika kila kaunti kuwe na hela ambazo zimetengwa ili kuwasaidia kuenda shule na kuhamasisha jamii kuhusu madhara ya kuwatenga watu walemavu na kujua ni vipi wataweza kuhusishwa. Hii ni kwa sababu wakati huu tunaona kwamba pesa nyingi zimewekwa tu katika Baraza la Kitaifa kuhusuWatuWalemavu. Lakini kama ambavyo imesemekana, Bodi ya Baraza hilo haijateuliwa karibu mwaka mzima sasa. Hili Bunge lilipeana Kshs1.3 bilioni mwisho wa makadirio ya matumizi ya Serikali na hizo hela hasijatumika. Masuala ya watu walemavu si tu masuala ya Serikali ya Kitaifa bali ni masuala ya serikali za ugatuzi. Kwa hivyo, ni lazima magavana na bunge za kaunti tofauti ziweze kuweka pesa ambazo zitasaidia watu walemavu."
}