GET /api/v0.1/hansard/entries/429211/?format=api
HTTP 200 OK
Allow: GET, PUT, PATCH, DELETE, HEAD, OPTIONS
Content-Type: application/json
Vary: Accept

{
    "id": 429211,
    "url": "https://info.mzalendo.com/api/v0.1/hansard/entries/429211/?format=api",
    "text_counter": 37,
    "type": "speech",
    "speaker_name": "Hon. (Ms.) Chidzuga",
    "speaker_title": "",
    "speaker": {
        "id": 751,
        "legal_name": "Zainab Kalekye Chidzuga",
        "slug": "zainab-kalekye-chidzuga"
    },
    "content": "Ahsante Mhe. Naibu Speaker. Langu ni pendekezo kwa Bodi ambayo inahusika na mikopo kwa wanafunzi. Hii ni kwa sababu tunaona, kwa mfano, katika sehemu ya Kwale, tunaweza kumaliza mihula kama miwili au mitatu na hakuna mtoto hata mmoja ambaye amepata mkopo huo. Hii ni keki ya Wakenya wote na inafaa igawanywe sawasawa ndiyo kila mahali watu wapate. Tungependa tujue ni mikakati ngani ambayo wameiweka ili kila sehemu ya nchi iweze kupata pesa hizo, ili watoto wetu waweze kusonga mbele na elimu. Hii ni kwa sababu vyuo vikuu vipo hata sehemu za nyanjani."
}