GET /api/v0.1/hansard/entries/429429/?format=api
HTTP 200 OK
Allow: GET, PUT, PATCH, DELETE, HEAD, OPTIONS
Content-Type: application/json
Vary: Accept

{
    "id": 429429,
    "url": "https://info.mzalendo.com/api/v0.1/hansard/entries/429429/?format=api",
    "text_counter": 255,
    "type": "speech",
    "speaker_name": "Hon. S.A. Ali",
    "speaker_title": "",
    "speaker": {
        "id": 2100,
        "legal_name": "Shariff Athman Ali",
        "slug": "shariff-athman-ali"
    },
    "content": "Ahsante, Bw. Naibu Spika wa Muda, kwa kunipa fursa hii ili niweze kuichangia Hotuba ya Rais. Ningependa kuchukua fursa hii kumpongeza Rais kwa kutekeleza majukumu yake ya kuja na kutuelezea maendeleo ambayo Serikali yake imefanya katika muda wa mwaka mmoja uliopita. Ni muhimu tufahamu kwamba katika nchi hii tuna matatizo. Ni matatizo ambayo Rais ameyakubali. Ni matatizo ambayo tunakumbana nayo kila siku. Nilifurahi Rais aliposema kwamba barabara ya kutoka Lamu kwenda Turkana, kwa sababu ya bandari ya Lamu, iko kwenye mipango ya Serikali. Masikitiko makubwa ni kwamba Serikali inazingatia kujenga barabara hiyo huku matatizo yanayowakumba wakazi wa Lamu kuhusiana na bandari hiyo yakipuuzwa. Serikali haijaweza kuyatatua matatizo ambayo yako Lamu. Kuna watu ambao wamefurushwa kutoka ardhi yao lakini The electronic version of the Official Hansard Report is for information purposesonly. A certified version of this Report can be obtained from the Hansard Editor."
}