GET /api/v0.1/hansard/entries/429431/?format=api
HTTP 200 OK
Allow: GET, PUT, PATCH, DELETE, HEAD, OPTIONS
Content-Type: application/json
Vary: Accept

{
    "id": 429431,
    "url": "https://info.mzalendo.com/api/v0.1/hansard/entries/429431/?format=api",
    "text_counter": 257,
    "type": "other",
    "speaker_name": "",
    "speaker_title": "",
    "speaker": null,
    "content": "mpaka sasa hakuna hata mtu mmoja ambaye amepewa fidia. Watu hao hivi sasa hawajielewi. Hawajui wafanye nini, ama waende wapi. Bw. Naibu Spika wa Muda, kuhusu masuala ya IDPs, ningependa kusema kwamba wakazi wa Lamu ndio walikuwa IDPs wa kwanza katika nchi hii. Kuna watu ambao walikuwa wakiishi katika maeneo ya Rubu na Mwombore. Hivi sasa watu hao wameondoka kutoka maeneo hayo. Wamekuwa IDPs. Mpaka sasa Serikali inazungumzia IDPs wa hivi majuzi bila ya kuwazungumzia IDPs wa kitambo. Kutokana na haya, ni lazima Serikali iwajibike na kujua kwamba tuna matatizo, na itafute njia mwafaka ya kuyatatua kabla ya kufanya mambo mengine. Tukizunguumzia masuala ya usalama, ni wengi waliochangia masuala hayo. Sote tutakubaliana kwamba usalama ni kama mlango wa nchi hii. Bila ya nchi hii kuwa na mlango, sidhani kwamba kutakuwa na mwelekeo wowote. Hivi sasa tunaona watu wakiuawa barabarani bila ya sababu zozote. Kuua na kuuawa limekuwa jambo la kawaida ambalo limeingia kwenye nyoyo za watu. Limekuwa jambo la kawaida. Ni masikitiko makubwa kuona kwamba viongozi, ama watu mashuhuri, katika nchi hii wanaweza kuuawa barabarani huku Serikali ikisema kwamba inafanya uchunguzi bila ya uchunguzi huo kujulikana ulipofikia na bila ya suluhisho lolote kupatikana. Tunaelekea mahali pabaya. Inafaa Serikali iliangazie suala hili, na kuchukua hatua kuhakikisha kwamba mambo haya yamewekwa katika uthibiti maalumu ili kuweza kuikomboa na kuitetea nchi hii katika siku za usoni. Mhe Rais na naibu wake wanazungumzia masuala ya uchumi wa nchi hii. Wanasema kwamba wameweza kupiga hatua na kuinua uchumi wa nchi hii. Masikitiko makubwa ni kwamba Wakenya, ambao wanaishi katika nchi hii, wanaamuka asubuhi wasijue wale nini ama waende wapi. Kwa kweli, katika nchi hii bado kuna watu ambao wana matatizo ya kiuchumi, na ambao hawajui wafanye nini. Tukizungumzia suala la mataniti, mhe. Rais amesema kwamba dada zetu na akina mama wajifungue bure katika hospitali za umma. Sijui kama ameweza kutembelea mataniti kwenye hospitali za umma na kuona jinsi zilivyo. Katika sehemu za mashinani kuna matatizo makubwa. Kwa hivyo, haifai kusema tu kwamba umefanya nini. Ni lazima Serikali iwajibike na kufuatilia masuala hayo."
}