GET /api/v0.1/hansard/entries/429461/?format=api
HTTP 200 OK
Allow: GET, PUT, PATCH, DELETE, HEAD, OPTIONS
Content-Type: application/json
Vary: Accept
{
"id": 429461,
"url": "https://info.mzalendo.com/api/v0.1/hansard/entries/429461/?format=api",
"text_counter": 287,
"type": "speech",
"speaker_name": "Hon. Murungi",
"speaker_title": "",
"speaker": {
"id": 2802,
"legal_name": "Kathuri Murungi",
"slug": "kathuri-murungi"
},
"content": "Kwa hivyo, nikiendelea nilikuwa nasema kwamba labda wale wenzangu wa CORD wananishuku. Ninazungumza kwa Kiswahili ndio kila mtu hata mama mboga asikie vile ninasema saa hii. Nasema labda kuna wale wanashuku Serikali haijafanya kazi yoyote. Kama kiongozi anasema hivyo, mbona tunashuku? Nitaendelea kusema kwamba miundo mbinu msingi ndio itasaidia nchi yetu; tumeona Rais amesema kwamba reli kutoka Mombasa mpaka Nairobi baadaye itaenda Malaba."
}