GET /api/v0.1/hansard/entries/429474/?format=api
HTTP 200 OK
Allow: GET, PUT, PATCH, DELETE, HEAD, OPTIONS
Content-Type: application/json
Vary: Accept
{
"id": 429474,
"url": "https://info.mzalendo.com/api/v0.1/hansard/entries/429474/?format=api",
"text_counter": 300,
"type": "speech",
"speaker_name": "Hon. Murungi",
"speaker_title": "",
"speaker": {
"id": 2802,
"legal_name": "Kathuri Murungi",
"slug": "kathuri-murungi"
},
"content": "Bw. Naibu Spika wa Muda, nasema labda Mhe. Ngong’o hana laini nzuri ya kufikia mkubwa wake; kwa hivyo nitaendelea kusema kwamba kile kitu Rais aligusia, na naona kitasaidia Kenya, ni wajibu wa kuhakikisha kwamba wawindaji haramu wamekamatwa na kufungwa. Leo tukizungumza kila mtu anaelewa kwamba wawindaji haramu wameuwa ndovu wetu na vifaru. Kwa hivyo, kulingana na zile sera Serikali imeweka sina wasiwasi kabisa kwamba tutaweza kukamata wale wakora na wale watu ambao wanaharibu nchi yetu. La mwisho ni kwamba ile asilimia 30 ambayo imepewa vijana, akina mama na walemavu, kuna sheria nyingi zimewekwa na Wizara ya Ugatuzi na Mipango. Kwa hivyo, ninaomba hiyo Wizara iangalie na iache kuitisha vyeti vya kuonyesha kama umelipa kodi ama ushuru. Kwa hivyo, haya mambo yote yakiangaliwa, nchi yetu itaendelea kuimarika."
}