GET /api/v0.1/hansard/entries/429480/?format=api
HTTP 200 OK
Allow: GET, PUT, PATCH, DELETE, HEAD, OPTIONS
Content-Type: application/json
Vary: Accept
{
"id": 429480,
"url": "https://info.mzalendo.com/api/v0.1/hansard/entries/429480/?format=api",
"text_counter": 306,
"type": "other",
"speaker_name": "",
"speaker_title": "",
"speaker": null,
"content": "Kiislamu wakiuawa. Ni sababu gani husika haswa ambayo inafanya usalama kudorora katika nchi yetu? Pia tusisahau kuangalia kuelewa kwamba kumekuwa na biashara ya silaha ndogo ndogo katika mipaka yetu. Je, vitengo vyetu vya kiusalama vimeangalia swala hili? Ni vipi Wakenya wengi wanaweza kupata silaha na kuweza kuathiri maisha ya Wakenya? Tunasikitika pia kuona kwamba vyombo vya usalama wakati kumetokea matukio kama ya Likoni--- Kuna wakati ambapo Makamu wa Rais alisema vijana wawili kati wale walioingia katika kanisa lile na kufanya visa vile, walikuwa wameuawa. Lakini je, kama Wakenya, tumeambiwa ni kina nani na wametoka sehemu gani? Tunapopata habari kama hii ndio tutaweza kujua kabisa watu hao walitoka upande gani. Kwa hivyo, tunaomba Serikali ituambie ni kina nani na walitoka wapi na ni watu wa aina gani. Jambo lingine ambalo nataka kuzungumzia ni kwamba Rais alizungumzia kwamba mahakama zimekuwa zikisaidia kuhakikisha kwamba taasisi zetu zimekuwa na usawa wa kijinsia. Hivyo basi napenda kuwaambia Wabunge wenzangu, haswa wale ambao wanataka kuleta Mswada wa kuondoa zile nafasi za akina mama 47, wakati watafanya hivyo watakuwa hawafuati ile falsafa ya vyama vyao na pia Katiba. Kama tunafuata Katiba, lazima tuangalie kwa undani mambo ya usawa wa jinsia. Jambo la tatu napenda kuzungumzia ni mradi wa reli na upanuzi wa bandari ya Mombasa, ambayo Rais amezungumzia. Iwapo jambo hili litatekelezwa kwa haraka na zile Wizara husika, basi tutaweza kupata ajira nyingi kwa vijana wetu na kuboresha utendaji kazi katika bandari ya Mombasa; hivyo basi uchumi wetu utaweza kukua zaidi. Jambo lingine ambalo Rais hakulizungumzia na ni swala nyeti sana ni kuhusu ajira. Nilitarajia Rais azungumzie vipi tutaweza kufufua viwanda ambavyo vimedorora na vingine hata kufungwa. Viwanda kama vya Bixa, korosho, makonge na pamba vinahitaji kuboreshwa ili tuweze kupata ajira kwa vijana wetu. Pia, inafaa tuboreshe sekta ya jua kali ili tuweze kuwa na ajira zaidi. Jambo la mwisho ambalo ningependa sana kuzungumzia kuhusiana na Hotua ya Rais ni bei za vyakula. Bei imepanda sana na Wakenya wengi wameshindwa hata kujimudu kimaisha katika upande wa chakula na mambo mengine. Ningependa kusema Serikali hii na sisi tukiwa ndani kama Wabunge tuweze kuangalia mambo ya kulipa ushuru wa VAT---"
}