GET /api/v0.1/hansard/entries/429533/?format=api
HTTP 200 OK
Allow: GET, PUT, PATCH, DELETE, HEAD, OPTIONS
Content-Type: application/json
Vary: Accept

{
    "id": 429533,
    "url": "https://info.mzalendo.com/api/v0.1/hansard/entries/429533/?format=api",
    "text_counter": 359,
    "type": "speech",
    "speaker_name": "Hon. (Ms.) Machira",
    "speaker_title": "",
    "speaker": {
        "id": 769,
        "legal_name": "Jane Agnes Wanjira Machira",
        "slug": "jane-agnes-wanjira-machira"
    },
    "content": "Ahsante Bw. Naibu Spika wa Muda kwa kunipa ruhusa ili nami niongee kidogo kuhusu Hotuba ya Rais. Rais Uhuru ametueleza kuhusu mpangilio wake wa kazi ili kutujulisha mambo anayofikiria kuhusu nchi yetu. Rais Uhuru ameshateua watu ambao tunaweza kusema ni watu ambao kazi yao ni ya mkono katika nchi nzima, nao ni Mawaziri. Tunaposema kwamba Rais hafanyi kazi labda kuna watu ambao wamesinzia katika nyadhifa zao. Tusitupe mawe kwa Rais tukisema kuwa hajafanya kazi yoyote. Rais alitujulisha mpangilio wake katika usalama. Aliteua nyumba kumi. Hii itatusaidia katika kuimarisha usalama. Huenda katika miji nyumba kumi isifaulu sana lakini mashinani najua zinaweza. Tukisema kwamba Rais hajafanya chochote tukumbuke zile nyadhifa ambazo inambidi kuteua watu ni chache mno. Sisi Wakenya tuna makabila 42 na tusingeweza kupata sote nafasi hizo. The electronic version of the Official Hansard Report is for information purposesonly. A certified version of this Report can be obtained from the Hansard Editor."
}