GET /api/v0.1/hansard/entries/436377/?format=api
HTTP 200 OK
Allow: GET, PUT, PATCH, DELETE, HEAD, OPTIONS
Content-Type: application/json
Vary: Accept

{
    "id": 436377,
    "url": "https://info.mzalendo.com/api/v0.1/hansard/entries/436377/?format=api",
    "text_counter": 238,
    "type": "other",
    "speaker_name": "",
    "speaker_title": "",
    "speaker": null,
    "content": "waliochaguliwa kuangalia kesi hii tena kulingana na sheria na haki za yule ambaye ameshtakiwa, wanaweza kumlinda? Hilo ndilo swali ambalo sisi kama Bunge ya Seneti yafaa tujiulize. Jambo la kwanza, hata ndani ya mahakama yule hakimu ambaye alikupata na hatia na kwa bahati mbaya ama nzuri ukakata rufani na ukaambiwa rudi chini usikizwe tena, ukirejeshwa kwa hakimu huyo tena, haki yako iko wapi mbele yake? Wewe uko na nafasi ya kumuuliza hakimu yule ajitenge kando ili kesi isikizwe na mwingine. Hiyo ndiyo haki. Hili Bunge la Seneti ni Bunge muhimu sana katika macho ya Wakenya. Inajulikana kwamba tunatekeleza haki. Wako Maseneta 47 na wale wengine wa maalum lakini tunasema kwamba kuna Maseneta zaidi ya 60. Hivi sasa tuko na hawa 11 ambao walikuwa wakimsikiliza Bw. Wambora hapo awali. Tunaweza kusema kwamba hii si ile kesi ya zamani lakini macho ya Wakenya inaona aje? Sisi kama Bunge la Seneti tuna haki ya kutekeleza haki."
}