GET /api/v0.1/hansard/entries/436381/?format=api
HTTP 200 OK
Allow: GET, PUT, PATCH, DELETE, HEAD, OPTIONS
Content-Type: application/json
Vary: Accept
{
"id": 436381,
"url": "https://info.mzalendo.com/api/v0.1/hansard/entries/436381/?format=api",
"text_counter": 242,
"type": "speech",
"speaker_name": "Sen. Madzayo",
"speaker_title": "",
"speaker": {
"id": 679,
"legal_name": "Stewart Mwachiru Shadrack Madzayo",
"slug": "stewart-mwachiru-shadrack-madzayo"
},
"content": "Asante ndugu yangu Sonko lakini ningependa kukueleza kwamba mshtakiwa ana njia mbili katika sheria. Mshtakiwa anaweza kukubali ama kukata rufaa. Kwa hivyo, jukumu hilo ni lake. Ningependa kusema kwamba sisi kama Seneti, ni Bunge ambalo linaheshimiwa katika Kenya nzima. Ikiwa kuna Mkenya ambaye haki yake haitatimizwa kwa sababu tumeamua ni lazima mambo yawe hivyo, kwa maoni yangu, naona haki haitatimizwa ikiwa tutaweka majina haya vile yalivyokuwa. Kuna umuhimu wa Maseneta hawa 11 kujiondoa ili Seneti iwachague wengine ambao akili zao hazijaamua. Hii ni kwa sababu kisheria, akili zao zimeshaamua na zinajua mwelekeo zinaotaka kufuata. Maseneta wengine wanafaa kuchaguliwa kuchunguza swala hili."
}