GET /api/v0.1/hansard/entries/436619/?format=api
HTTP 200 OK
Allow: GET, PUT, PATCH, DELETE, HEAD, OPTIONS
Content-Type: application/json
Vary: Accept
{
"id": 436619,
"url": "https://info.mzalendo.com/api/v0.1/hansard/entries/436619/?format=api",
"text_counter": 180,
"type": "speech",
"speaker_name": "Sen. (Dr.) Machage",
"speaker_title": "",
"speaker": {
"id": 179,
"legal_name": "Wilfred Gisuka Machage",
"slug": "wilfred-machage"
},
"content": "Bw. Spika, muda wa dakika tatu si mwingi, lakini nitautumia kutoa wasia wangu na labda kuwapa mawazo wale viongozi wa mashinani, hasa magavana. Wahenga walisema: “Ukiona cha mwenzio cha nyolewa, chako kitie maji.” Pia walisema: “Asiyeskia la mkuu, huvunjika guu.” Leo tunajaribu kuangaza mawazo yetu juu ya Ripoti iliyotayarishwa na Kamati ya Sen. (Dr.) Khalwale. Mambo yote juu ya Kaunti ya Embu yameanikwa wazi. Tunaweza kudhibitisha kwamba kuna dosari katika usimamizi wa mali ya umma katika kaunti hii. Juzi nimejaribu kumtetea Gavana Wambora na kumpa nafasi ili ajitetee. Yeye akadinda hata kufika mbele ya Kamati ya Seneti iliyoundwa na Seneti hii. Sina budi ila kusema ya kwamba yeye hafai kuwa kiongozi wa daraja lolote kwa sababu amekosa utiifu. Ingekuwa heri kama angekubali kusikiza mawazo ya viongozi wa Seneti hii. Je, atawezaje kuongoza wananchi wa Kenya ikiwa hana utiifu? Bw. Spika, ningetaka kutoa tahadhari juu ya mambao yanayotendeka wakati huu kule mashinani. Magavana wengi ambao wanajua wana makosa kama yale ya Gavana Wambora wameanza kutoa rushwa au mlungula kwa wale viongozi wa mashinani wanaojulikana kama MCAs. Ni lazima wajue ya kwamba twawakodolea macho na tunawachunguza. Hatutakubali mambo ya hongo kabisa katika Seneti hii. Ni vibaya kutumia pesa za umma kuwahonga viongozi wengine ili wafiche maovu yao. Iwapo wataletwa hapa, basi kisu ni kile kile na wembe ni ule ule!"
}