GET /api/v0.1/hansard/entries/437155/?format=api
HTTP 200 OK
Allow: GET, PUT, PATCH, DELETE, HEAD, OPTIONS
Content-Type: application/json
Vary: Accept
{
"id": 437155,
"url": "https://info.mzalendo.com/api/v0.1/hansard/entries/437155/?format=api",
"text_counter": 389,
"type": "speech",
"speaker_name": "Sen. Muthama",
"speaker_title": "",
"speaker": {
"id": 96,
"legal_name": "Johnson Nduya Muthama",
"slug": "johnson-muthama"
},
"content": "Bw. Naibu Spika, mimi nasimama hapa nikiwa na uzito sana. Uzito umenizidi. Ninatafuta mlango wa kupitia ili niunge mjadala huu na mazungumzo haya mkono lakini nimeshindwa na nimelemewa. Najilazimisha kwa sasa kuguzia mambo mawili tu. Bw. Naibu Spika, kile kiti nilikuwa nakalia na hicho ambacho umekalia kina majukumu yake na kimepangiwa kazi yake. Ukitoa uamuzi wako tunakubali na tunaitikia. Hapa tumekuwa na mchezo wa kwenda mbele na kurudi nyuma. Sisi tumeweka tume ya kuweka kielelezo na njia ya kupanga vile pesa zetu zitagawa katika kaunti zetu. Tume ya CRA ambayo makamishma wake wanalipwa pesa na wananchi na sisi hapa, Katiba inasema wakisie kiwango cha pesa na walete kwetu. Kwa mara mbili hao watu wamekaa, wakafanya kazi yao ya kukisia na wakaleta hapa. Mara ya kwanza tulitupa nje waliyoleta. Swali ni kwamba, kwa nini wachukue mshahara kwa kufanya kazi ambayo haikubaliwi? Jambo la pili ni kwamba wametoa makisio ya mwaka huu. Watu fulani waliketi wakiwa na kamati ya kupanga mambo ya fedha wakaleta ujumbe The electronic version of the Senate Hansard Report is for information purposes only. A certified version of this Report can be obtained from the Hansard Editor, Senate."
}