GET /api/v0.1/hansard/entries/437157/?format=api
HTTP 200 OK
Allow: GET, PUT, PATCH, DELETE, HEAD, OPTIONS
Content-Type: application/json
Vary: Accept
{
"id": 437157,
"url": "https://info.mzalendo.com/api/v0.1/hansard/entries/437157/?format=api",
"text_counter": 391,
"type": "other",
"speaker_name": "",
"speaker_title": "",
"speaker": null,
"content": "kusema kwamba zile pesa wametoa na wamekisia, zimerudishwa chini. Hatujui ni nani amefanya hiyo kazi na hatujui wao watakuwa na raha na heshima gani ya kufanyia taifa hili kazi. Bw. Naibu Spika ukiangalia katika mgao wa mwaka uliopita, hesabu ambao ilitumika ilikuwa ya mwaka wa 2010/2011. Sasa huu ni mwaka wa nne. Hivi sasa haieleweki hizi pesa ambazo zimepangwa ni za mwaka gani lakini chini yake imeandikwa “2009/2010”. Katiba inasema kwamba kitakachotumika ni makisio ya hesabu iliyofanyika mwisho. Sasa ya mwisho ni 2009/2010 ama ni 2010/2011? Je, tunaenda mbele au nyuma? Tukipitisha Mswada huu ukiwa hivi kutakuwa na sarakasi na mchezo wa paka na panya. Mwaka ujao itakuwa zaidi ya hii kwa sababu tutakalishwa hapa na kuambiwa kwamba mwaka uliyopita mlipitisha hivyo. Itakuwaje kwa watu ambao wanaweza kuona na kufanya hesabu hiyo kufanya hivyo? Je, mwenye kuandika haya na kusema kwamba ni asilimia 43 alisema ni ya pesa gani? Hakuna ambaye anajua hilo. Bw. Naibu Spika, CRA wamesema kwamba tupewe Kshs279.162 billioni ambayo ni asilimia 26. Ikiwa uchumi wetu kwa kweli umekuwa ni asilimia 11, yafaa tupate Kshs300 billioni, lakini sasa tuko chini ya Kshs279. Swali ni hili; uchumi huu umekuwa kwa maneno au ni kihalali? Kama ni halali mimi sioni kwa nini tukae hapa tuongee asilimia tano ya pesa tulizopata mwaka uliyopita. Ni dhahiri kwamba bali na kupewa pesa na hesabu ya miaka mitatu nyuma, kwa hali ya ukweli pesa zinazotolewa ni za mwaka huu. Pesa ambayo itatolewa ni ya akiba ya kitaifa ya mwaka huu. Kwa hivyo, ukichukua pesa ambazo zinakisiwa, huu ndio ukweli wa mambo, kutoka kwa Kshs1.6 trillioni ukitoa Kshs226 billion, Serikali inabaki na kitita cha karibu Kshs1.4 trillioni. Sasa tunaenda wapi sisi kama taifa, na tunaenda kuambia watu wetu nini? Ikiwa pesa hizi zina baki katika Serikali kuu; kutoka Rais, Makamu wa Rais; awe nani au nani, kila mtu anatoka katika kaunti. Juzi tumeshuhudia Rais mwenyewe akisema kuwa alipoingia katika Ofisi ya Rais, karibu Kshs300 bilioni zilikuwa haziwezi kuhesabika. Sen. Wangari hapa amegusia na kusema kwamba ikiwa itatajwa na kutamkwa kwamba kiasi cha Kshs500 kinaweza kupotea kwa njia ya magendo na rushwa, halafu zile pesa ambazo wananchi wanaweza kwenda na kuangalia kwa karibu na macho yao, nazo ni pesa zinazotoka katika kaunti zinakatwa; na ile inabaki, inabaki pale ambapo kuna panya, kunguni na mchwa kutafuna, je, sisi tunaenda kufanya nini? Lengo la Katiba mpya lilikuwa ni kutoa mambo hayo. Kazi hii kutoka kwa Serikali Kuu kukupangia eti Murang’a mutapata Kshs100 bilioni, na hakuna kitu kinafika; au mutapata Kshs100 milioni huko Baringo, na hakuna kitu kitafika; tukaleta Katiba hii ambayo tuliiuza Wakristo huku wakiikataa--- Mimi niliiuza nani alimkuta kasisi wa kanisa la Katoliki akipeana sakramenti huku akisema “kula sakramenti na usisahau Katiba ni mbaya.” Nilikua katika kanisa hilo nikingojea misa iishe ili “niuze” Katiba; hakuna kazi ilikuwa ngumu kama hiyo! Niliifanya hiyo kazi ili nihakikishe kwamba pesa hizi zinafika mashinani na wananchi wanakaa chini ili kupanga matumizi yake. Haya nimachungu mazito! Napinga Mswada huu na nitapiga kura kuukataa. Nasema kuwa ni Kshs279 bilioni zilizopangwa na Commission for Revenue Allocation (CRA), na yule mtu ambaye anasema tu na kukanusha yale maoni yaliyotolewa na CRA watuambie tutaenda kwa nani. Ikiwa hawa The electronic version of the Senate Hansard Report is for information purposes only. A certified version of this Report can be obtained from the Hansard Editor, Senate."
}