GET /api/v0.1/hansard/entries/437170/?format=api
HTTP 200 OK
Allow: GET, PUT, PATCH, DELETE, HEAD, OPTIONS
Content-Type: application/json
Vary: Accept
{
"id": 437170,
"url": "https://info.mzalendo.com/api/v0.1/hansard/entries/437170/?format=api",
"text_counter": 404,
"type": "speech",
"speaker_name": "Sen. Muthama",
"speaker_title": "",
"speaker": {
"id": 96,
"legal_name": "Johnson Nduya Muthama",
"slug": "johnson-muthama"
},
"content": "Bw. Naibu Spika, nataka kusema hapa leo kwamba yafaa tupeane heshima na kila mtu apewe nafasi ili afanye kazi yake. Rais yuko na kazi yake; kwa hivyo tumpe heshima na wakati ili aifanye hiyo kazi. Sisi hapa kama Seneti tuko na kazi yetu; CRA wako na kazi yao, na kama hawana kazi, mimi nasema tuwafute kazi ili waende nyumbani! Kwa nini wakae katika ofisi, wanafanya kazi usiku na mchana; wanapanga pesa, halafu tunafika hapa na kusema “Aa, ile kazi wamefanya haifai; ile tu ndio inafaa?” Katiba ingejua kwamba sisi tuko na uwezo huo, basi tungelifanya kazi hiyo. La mwisho, Bw. Naibu Spika, tulienda katika Supreme Court na korti ikaamua kwamba ni sisi Seneti ambayo nikielelezo na ina uwezo wa kuamua pesa itatoka wapi na kwenda namna gani. Hivi sasa, tunarudi tena kukaa nyuma ya Bunge nakusema “Bunge imetoa; tukianguka tutapata aibu.” Aibu gani tutapata kama tunakaa hapa na kusema “Bunge mumekosea na muliyofanya hayafai?” Bw. Naibu Spika mimi nimeudhika sana na napinga Mswada huu!"
}