GET /api/v0.1/hansard/entries/437214/?format=api
HTTP 200 OK
Allow: GET, PUT, PATCH, DELETE, HEAD, OPTIONS
Content-Type: application/json
Vary: Accept

{
    "id": 437214,
    "url": "https://info.mzalendo.com/api/v0.1/hansard/entries/437214/?format=api",
    "text_counter": 448,
    "type": "speech",
    "speaker_name": "Sen. Chiaba",
    "speaker_title": "",
    "speaker": {
        "id": 3,
        "legal_name": "Abu Mohamed Chiaba",
        "slug": "abu-chiaba"
    },
    "content": "Bw. Naibu Spika, sikio la kufa halina dawa. Hivi sasa, tuko na Katiba mpya inayotupa haki ya kupata pesa sawa katika kaunti zote. Huo ndio wajibu mkubwa wa Bunge hili la Seneti. Lakini kwa miaka hii yote miwili iliyopita, Bunge hili haliwezi kujivunia ya kwamba wametupa pesa za kutosha katika kaunti yetu. Tumeletewa yale makadirio ya kwanza na yakapita; tukafanya mapendekezo ya Seneti yakapuuzwa na mapendekezo ya watu wengine yakachukuliwa. Hivi sasa, tunaulizwa kupitisha Kshs226 bilioni. Hata mimi ninaunga mkono Mswada huu huko kama nimefunga jicho moja."
}