GET /api/v0.1/hansard/entries/439121/?format=api
HTTP 200 OK
Allow: GET, PUT, PATCH, DELETE, HEAD, OPTIONS
Content-Type: application/json
Vary: Accept
{
"id": 439121,
"url": "https://info.mzalendo.com/api/v0.1/hansard/entries/439121/?format=api",
"text_counter": 349,
"type": "speech",
"speaker_name": "Sen. Muthama",
"speaker_title": "",
"speaker": {
"id": 96,
"legal_name": "Johnson Nduya Muthama",
"slug": "johnson-muthama"
},
"content": "Bw. Naibu Spika, nimesema viongozi wanafaa kuongoza watu wakiwaelekeza mahali wanapofaa kuenda. Sijasema eti hawafai kuwauliza. Hata wakiwa kwa njia, wananchi wanaweza kuuliza ni wapi wanapopelekwa na kiongozi ana haki ya kuwaambia; ninawapeleka mahali mnastahili kuwa. Hakuna mtu anazuiliwa kuuliza swali. Tumekuwa na viongozi ambao hawafanyi bajeti. Pia, hawafanyi hesabu vizuri. Wanatumbukizia wananchi mambo ambayo wanataka yawafurahishe watu wao. Tumeshuhudia mambo mengi. Tusiposimama kama Seneti ambalo lina jukumu la kuingoza nchi, hatutaweza kuyalainisha mambo na kuyaweka vile yanatakiwa kuwa. Ni lazima tuongoze kwa kusema mambo ambayo yanastahili. Bw. Naibu Spika, hivi karibuni, tulikuwa pamoja kule Berlin. Nchi ya Ujerumani iko mbele katika maendeleo na asilimia nyingi mno mbele ya nchi yetu. Tunavyozungumza sasa, mambo yanayoendelea Munich na yale yanayoendelea Frankfurt hayafanani. Uchumi wa Berlin pia hauwezi kufananishwa na jiji zingine. Jiji la Berlin ndio makao makuu ya nchi ya Ujerumani. Dodoma ilistahili kuwa jiji kuu la Tanzania kwa maneno lakini marehemu Nyerere angekuwa hai, kwa vile alikuwa msema kweli, angesema, hata kama hakukosea, alikuwa karibu kukosea. Dodoma, hata leo, bali na kuwa na Bunge la Kitaifa, hakuna kitu kingine ambacho huendelea huko. Wananchi wa Tanzania hutembea sana kutoka sehemu kama vile Dar es Salaam, Moshi na Arusha kuenda Dodoma lakini jiji hilo bado liko chini. Nilikuwa Abuja hivi karibuni. Ukimuuliza Mnaijeria sababu ambayo inayoweza kufanya aende Abuja, atakwambia yeye huenda Abuja kumuona Waziri wake lakini hana sababu nyingine ya kuenda huko. Tuseme ukweli hapa. Magavana wengine wetu wamekosea katika mambo mengi. Mimi ni mwekezaji katika eneo la Taita Taveta. Ukiangalia mahali ambapo gari hukuweka, utashangaa sana kwa sababu mji ambao ulio karibu na hapo, ambao uko 260 kilomita ni Mwatate. Mji mwingine ulio karibu ni Wundanyi ambao uko 85 kilomita. Kuna marumbano ambayo hatujaona huko Taita Taveta. Wajumbe na MCAs wamegawanyika. Gavana anataka kuhamisha makao makuu ya kaunti mahali panapoitwa Mugeni. Mugeni ni 115 kilomita. Kwa sababu yeye ameamua, kuna shida. Hata tukipitisha Mswada huu, hiyo haizuii watu kubadilisha nia wakiona shida. Hayo ni mambo ambayo yanaweza kuzungumzwa na wananchi. Tunafaa kufanya mambo kwa heshima na adabu na tupunguze ndoto za wale watakuwa magavana na kutumia pesa vibaya wakijenga makao ya kaunti mahali wanapotaka. The electronic version of the Senate Hansard Report is for information purposes only. A certified version of this Report can be obtained from the Hansard Editor, Senate."
}