GET /api/v0.1/hansard/entries/439123/?format=api
HTTP 200 OK
Allow: GET, PUT, PATCH, DELETE, HEAD, OPTIONS
Content-Type: application/json
Vary: Accept

{
    "id": 439123,
    "url": "https://info.mzalendo.com/api/v0.1/hansard/entries/439123/?format=api",
    "text_counter": 351,
    "type": "other",
    "speaker_name": "",
    "speaker_title": "",
    "speaker": null,
    "content": "Tunafaa kukataa mambo ambayo yatachangia magavana kutumia vibaya pesa za kaunti. Katika kaunti yangu, Mavoko hutoa mchango mkubwa wa kodi ambayo hukusanywa kila mwezi. Kuna kiongozi mmoja aliyekuwa akitaka makao makuu ya Kaunti ya Machakos yapelekwe Mavoko. Ukiwa Mavoko, unakuwa karibu sana na Nairobi. Mtu ambaye anatoka Masinga na sehemu nyingine za ukambani atakuwa akija hadi Mavoko kutafuta huduma? Haya ni mambo ambayo sisi kama viongozi tunafaa tuyaangalie. Kama shida hii iko katika kaunti moja ama mbili, tunaweza kutatua shida hiyo ili tulinde raslimali ya Serikali na wananchi wa Kenya. Tunafaa kupitisha Mswaada ambao unasema Gavana hawezi kuhamisha makao makuu ya kaunti hadi sehemu yoyote. Hiyo italeta heshima na adabu."
}