GET /api/v0.1/hansard/entries/439214/?format=api
HTTP 200 OK
Allow: GET, PUT, PATCH, DELETE, HEAD, OPTIONS
Content-Type: application/json
Vary: Accept
{
"id": 439214,
"url": "https://info.mzalendo.com/api/v0.1/hansard/entries/439214/?format=api",
"text_counter": 33,
"type": "speech",
"speaker_name": "Hon. Simba",
"speaker_title": "",
"speaker": {
"id": 12532,
"legal_name": "Paul Simba Arati",
"slug": "paul-arati-simba"
},
"content": "Asante sana, Bw. Spika. Nataka nichukue nafasi hii nitume rambirambi zangu kwa wananchi wa Gatundu Kusini kwa sababu ya kumpoteza ndugu yetu, Mhe. Nyumu. Hayati Nyumu alikuwa rafiki wangu wa karibu sana wakati tulikuwa pamoja katika Kamati ya Elimu, Utafiti na Tekenolojia. Bw. Spika, nataka kusema mambo mawili kuhusu hayati ndugu yetu, Mhe. Nyumu. Hayati Mhe. Nyumu alilala akiwa ni kiongozi mchanga na ilikuwa mara yake ya kwanza kuingia katika Bunge hili. Tukiwa katika mkutano wa kwanza, katika chumba kidogo pale ndani, tuliguzia swala la Wabunge wale wa kwanza kupata malipo ya uzeeni. Akiwa mmoja wa wale wamelala; katika uongozi wake, huu ndio wakati ambapo tungeangalia swala la kupata malipo ya uzeeni, hata kama ni kuingia siku moja na uondoke katika Bunge hili. Bw. Spika, nataka kusema kwamba ingekuwa vyema kama wale waliokuwa katika safari rasmi kule nje, wangetoa msaada wao ili kuisaidia familia ya ndugu yetu Nyumu. Ninasikitika moyoni kwamba wale waliotutangulia humu ndani hawakuwa na mikakati kamili ya kuhakikisha kwamba tupo na njia mwafaka ya kukusanya fedha kidogo kidogo za kusaidia wakati kama huu; hata kama nikupitia kwa njia ya malipo ya check-off system. Ningeomba kwamba tuliangalie swala hili. Tuwe na kiwango fulani ambacho tutahitajika kutoa wakati kama huu, kinaweza kuwa shilingi 10,000 ama 20,000. Jambo hili litasaidia sana familia ya wale watakuwa wametuaga. Kwa wale wanashughulikia maslahi yetu, tungeomba kwamba washughulikie swala hili kwa sababu ya wale wenzetu ambao watatuacha kwa kifo. Mungu aibariki familia ya ndugu Nyumu na wale ambao alikuwa akiwawakilisha Bungeni. Asanta Sana."
}