GET /api/v0.1/hansard/entries/439231/?format=api
HTTP 200 OK
Allow: GET, PUT, PATCH, DELETE, HEAD, OPTIONS
Content-Type: application/json
Vary: Accept
{
"id": 439231,
"url": "https://info.mzalendo.com/api/v0.1/hansard/entries/439231/?format=api",
"text_counter": 50,
"type": "other",
"speaker_name": "",
"speaker_title": "",
"speaker": null,
"content": "na pia wenzangu katika Bunge hili. Marehemu Mhe. Ngugi alikua rafiki yangu, alikua mmoja wa watu wale ambao nilikuja kujuana nao baada ya kuchaguliwa na kuingia katika Bunge hili. Tulijiuliza ni vipi sisi kama Wabunge wapya tutaweza kusaidika. Wakati niliona mtu ambaye ni wa rika langu ametuacha, nikapata hofu kidogo kua kazi hii yetu labda wakati mwingine inatusukuma. Nafikiria heshima ile ambayo tunaweza kumpatia ndugu mwenzetu ambaye ametuacha ni kutimiza wajibu wetu sisi tulioachwa kwa bidii, na kuhakikisha Bunge hili linatimiza kazi yake. Naomba Mungu aipatie familia yake nguvu kustahimili kumpoteza ndugu yetu na pia waweze kua na amani. Tunaomba watu wa Gatundu waweze kupata mtu ambaye ataziba pengo lile ambalo limeachwa na marehemu ndugu yetu. Ahsante, Mhe. Spika."
}