GET /api/v0.1/hansard/entries/439877/?format=api
HTTP 200 OK
Allow: GET, PUT, PATCH, DELETE, HEAD, OPTIONS
Content-Type: application/json
Vary: Accept

{
    "id": 439877,
    "url": "https://info.mzalendo.com/api/v0.1/hansard/entries/439877/?format=api",
    "text_counter": 262,
    "type": "speech",
    "speaker_name": "Hon. (Dr.) Shaban",
    "speaker_title": "",
    "speaker": {
        "id": 139,
        "legal_name": "Naomi Namsi Shaban",
        "slug": "naomi-shaban"
    },
    "content": "Asante sana Mheshimiwa Naibu Spika wa Muda kwa kunipatia nafasi hii ya kuweza kuunga mkono mabadiliko haya na mapendekezo haya ya kubadilisha sheria ambayo inasimamia maswala kuhusu unywaji wa pombe hapa nchini. Nataka kuunga wenzangu mkono kwa kumpongeza Mheshimwa Ichung’wah kwa kuleta mabadiliko haya ambayo yataweza kusaidia zaidi watu wetu wengi ambao ni watumizi wa pombe. Pombe kwa wingi ni hatari kwa maisha. Pombe haswa kwa wengi wetu hatujaona umuhimu wa pombe lakini kwa wale ambao ni watumiaji wa pombe ambayo ni wapigaji kura wetu na ni Wakenya wenzetu, ningependa kusema ya kwamba kuna pombe ambazo ni za kienyeji ambazo kuna umuhimu wa hizo kupatiwa nafasi wananchi waweze kunywa bila wasiwasi wowote bora wasipitishe kiwango fulani. Sheria hii haswa inazungumzia maswala ya kuhakikisha kuwa kutaweza kuweko mipango kabambe na Serikali ya kuwezesha wale ambao wamezidiwa na shida hii na wenye kupenda kunywa pombe zaidi ya kiasi kuweza kusaidika. The electronic version of the Official Hansard Report is for information purposesonly. A certified version of this Report can be obtained from the Hansard Editor."
}