GET /api/v0.1/hansard/entries/439879/?format=api
HTTP 200 OK
Allow: GET, PUT, PATCH, DELETE, HEAD, OPTIONS
Content-Type: application/json
Vary: Accept
{
"id": 439879,
"url": "https://info.mzalendo.com/api/v0.1/hansard/entries/439879/?format=api",
"text_counter": 264,
"type": "other",
"speaker_name": "",
"speaker_title": "",
"speaker": null,
"content": "Mheshimiwa Naibu Spika wa Muda, na swala hili la kuweza kuwapatia sehemu ambazo wanaweza kuenda kupata matibabu ni muhimu sana. Maanake unywaji mwingi wa pombe kweli ni ugongjwa na pahali ambapo wataweza kuenda kupata matibabu bila kusumbuka na kuweza kurudia maisha yao ya kawaida na kuweza kujumuika na wenzao kwenye maendeleo ya nchi hii, swala hili ni swala ambalo tunatakikana kuliunga mkono. Mheshimiwa Naibu Spika wa Muda, pombe ambazo ndugu yetu Mbunge Kimani Ichung’wah hakutaja ni kama pombe za mnazi. Ndugu yangu, hayati Karisa Maitha alisema kwamba mnazi ni chakula. Ni kweli pombe inatoka kwa minazi na ni pombe ambayo inatumiwa katika maeneo ya Pwani. Pia, kuna pombe zinatengenezwa kutokana na asali, ndizi kama vile mbeke na busaa . Kuna pombe tofauti tofauti ambazo zinatumiwa na watu wetu hapa nchini. Pia ni pombe ambazo zinaweza kusaidia watu ili wasinunua zile pombe ambazo ni za bei ya juu. Bi. Naibu Spika wa Muda, wahenga walisema, “mwacha mila ni mtumwa.” Pombe hizi zimehusishwa sana kwa maswala ya kinyumbani, kama vile kulipa mahari na sherehe zote zinazoendelezwa nyumbani. Kwa hivyo, tuungeni mkono swala hili ili Serikali iweze kutengeneza maeneo ambayo wale wana matatizo makubwa wanaweza kusaidika. Lakini ukweli in kwamba, pombe nyingi ni hatari kwa maisha ya wale wanaokunywa; iwe ni pombe ya kienyeji ama pombe zile zetu tunatumia wakati tunafanya sherehe zetu. Tujue kwamba pombe ina hatari. Pombe inaumiza haswa maini ya binadamu na ikisha choma maini, maisha yanakuwa mafupi na hutaweza kuungana na wenzako. Bi. Naibu Spika wa Muda, ijapokuwa pombe ni hatari, ni maisha pia. Kwa vile wananchi wetu wamependekeza sana wapate kinywaji na kuburudika na kinywaji hicho, ninaomba kwamba wakati tunatengeneza haya yote, Wakenya wakunywe kwa kiasi; wasizidishe kwa sababu ukizidisha pombe itakuwa sumu. Asante sana, ninaunga mkono Mswada huu."
}