GET /api/v0.1/hansard/entries/440323/?format=api
HTTP 200 OK
Allow: GET, PUT, PATCH, DELETE, HEAD, OPTIONS
Content-Type: application/json
Vary: Accept
{
"id": 440323,
"url": "https://info.mzalendo.com/api/v0.1/hansard/entries/440323/?format=api",
"text_counter": 399,
"type": "speech",
"speaker_name": "Hon. Wekesa",
"speaker_title": "",
"speaker": {
"id": 2742,
"legal_name": "David Wafula Wekesa",
"slug": "david-wafula-wekesa"
},
"content": "moja kwa ripoti moja tu kwa sababu najua mengi yamesemwa kuhusu Mawaziri. Mimi ningependa kuongea kuhusu jambo moja. Kumekuwa na shida kuhusu idadi ya Wabunge Bungeni wakati wa asubuhi siku za Jumatano. Mara kwa mara tunapoungana humu Bungeni siku za Jumatano huwa tunakosa idadi inayohitajika ya Wabunge ili kuanza shughuli za siku. Hata hivyo, kamati hii ilipendekeza kwamba Bunge lianze shughuli zake za siku saa tatu na nusu asubuhi na kumaliza shughuli hizo saa saba mchana. Naomba kwamba tusijekufanya hayo mabadiliko kisha tuzidi kuwa na shida hiyo hiyo ya kukosa akidi. Hii ni kwa sababu machoni pa umma tutaonekana kuwa watu wasiotenda kazi. Kwa hayo machache naomba kuunga mkono Hoja hii."
}