GET /api/v0.1/hansard/entries/440458/?format=api
HTTP 200 OK
Allow: GET, PUT, PATCH, DELETE, HEAD, OPTIONS
Content-Type: application/json
Vary: Accept

{
    "id": 440458,
    "url": "https://info.mzalendo.com/api/v0.1/hansard/entries/440458/?format=api",
    "text_counter": 115,
    "type": "speech",
    "speaker_name": "Sen. Muthama",
    "speaker_title": "",
    "speaker": {
        "id": 96,
        "legal_name": "Johnson Nduya Muthama",
        "slug": "johnson-muthama"
    },
    "content": "Bw. Spika wa Muda nakushukuru sana kwa nafasi hii ili nichangie Hoja hii. Nimemsikiza kwa makini sana dada yangu, Sen. Elachi, akizungumza kuhusu mambo yanayohitajika katika mjadala huu. Pia nimewasikiza wale ambao wamezungumza kabla mimi. Bw. Spika wa Muda, ni dhahiri kwamba katika taifa letu hatujakuwa na shida na Umoja wa Mataifa. Majeshi yetu yametumika katika dunia nzima lakini la kushangaza ni kwamba unajaribu kuipaka mafuta Umoja wa Mataifa ili wanajeshi wetu waweze kupata kazi. Kule hakutafutwi kazi, wanajeshi wanaenda kule kukiwa na shida. Lakini kuna mambo ambayo yameharibika katika nchi yetu. Hivi majuzi, Jenerali Mulinge alikuwa Sierra Leone na aliweza kupata medali ya juu sana kutokana na msimamo wake wakati majeshi yetu yalitekwa nyara. Aliambiwa kuwa angeweza kuondoka, lakini alionyesha ujasiri wa majeshi ya Kenya, kwa kusema kuwa kamwe habanduki wala kuondoka hadi askari wake waachiliwe. Hiyo ndio njia ambayo tunataka kufuata. Bw. Spika wa Muda, aliyeleta Hoja hii anatoka upande wa Serikali. Labda ni kwa sababu anajua kuwa kuna shida fulani. Hoja hii inasisitiza Serikali kuzungumza na Umoja wa Mataifa ili tukubaliwe kuwa katika ngazi ya juu ya kufanya mambo haya. Aliyeleta Hoja hii angesema"
}