GET /api/v0.1/hansard/entries/440472/?format=api
HTTP 200 OK
Allow: GET, PUT, PATCH, DELETE, HEAD, OPTIONS
Content-Type: application/json
Vary: Accept

{
    "id": 440472,
    "url": "https://info.mzalendo.com/api/v0.1/hansard/entries/440472/?format=api",
    "text_counter": 129,
    "type": "speech",
    "speaker_name": "Sen. Muthama",
    "speaker_title": "",
    "speaker": {
        "id": 96,
        "legal_name": "Johnson Nduya Muthama",
        "slug": "johnson-muthama"
    },
    "content": "Bw. Spika wa Muda, Hoja hii inazungumzia mambo ya Umoja wa Mataifa. Inahimiza Serikali ya juu kuongea na Umoja wa Mataifa ili majeshi yetu yakubaliwe kushiriki katika shughuli za kurejesha amani ulimwenguni. Hayo ndio mambo ambayo yako ndani ya mjadala huu. Hatuwezi kuongea kuhusu uhusiano wa Kenya na Umoja wa Mataifa kama hatuongei kuhusu uhusiano wa uongozi wa Kenya na Umoja wa Mataifa. Hatuwezi kusema kuwa haya ni maji na hii na chupa. Maji yakiingia ndani ya chupa bado huitwa maji. Mimi sikusema kuwa kuna mtu ambaye amehukumiwa. Nimeongea kuhusu wizi uliofanyika katika Westgate. Pia, nimesema kwamba uongozi wa juu wa nchi hii una mashtaka katika Korti ya Kimataifa. Sikusema kuwa kuna mtu ambaye amehukumiwa au kupelekwa jela. Nimesema kwamba mashtaka yapo na kama kuna mtu anayeweza kusimama hapa na kusema kwamba hakuna mtu ambaye ana mashtaka kule, atakuwa anasema uwongo. Kwa hivyo, tupeane heshima na ukweli usemwe katika taifa hili. Bw. Spika wa Muda, nchi yetu haihitaji kuzungumza na kubembeleza Umoja wa Mataifa. Tunataka kuweka heshima ya taifa letu kutoka mtu wa juu hadi chini. Askari wetu wanafaa kuwa na adabu ya kufaa kutoka juu mpaka chini. Hiyo imewawezesha askari wetu kwenda kuhudumu katika nchi za nje kutoka wakati wa hayati Mzee Kenyatta, Moi na Kibaki. Bw. Spika wa Muda, napinga Hoja hii na kusema kwamba hatuhitaji kuwatafutia wanajeshi wetu kazi katika Umoja wa Mataifa. Tunataka Majeshi yetu yaende kule na kudumisha amani na utawala, vile tunafanya Somalia, Sudan Kusini na katika nchi zingine."
}