GET /api/v0.1/hansard/entries/440535/?format=api
HTTP 200 OK
Allow: GET, PUT, PATCH, DELETE, HEAD, OPTIONS
Content-Type: application/json
Vary: Accept
{
"id": 440535,
"url": "https://info.mzalendo.com/api/v0.1/hansard/entries/440535/?format=api",
"text_counter": 192,
"type": "other",
"speaker_name": "",
"speaker_title": "",
"speaker": null,
"content": "Bw. Spika wa Muda kule Lamu elimu ya chekechea hairidhishi hata kidogo. Shule zilikuwa katika hali mbovu. Hazina vifaa na walimu wa kutosha. Vile vile hakukuwa na vifaa vya kuchezea katika shule hiyo. Hali ya Lamu ilikuwa ni hatari. Bw. Spika wa Muda haina haja ya kuongeza kuhusu hali ya Tana River. Ukifika kule utafikiri kwamba labda haupo Kenya, baada ya miaka 50 ya Uhuru. Hili ni jambo ya kushangaza. Ukweli usemwe. Katika Kaunti ya Tana River, shule za chekechea na ufundi pia zilikuwa katika hali duni bin dhaifu. Huo ndio ukweli wa maneno. Bw. Spika wa Muda, pia tuliweza kukutana na Magavana katika kaunti hizo. Ningependa kumshukuru Mwenyekiti wa Kamati hii, Sen. Mutahi, ambaye hakuchoka. Tulitumia masaa saba kusafiri kutoka Lamu hadi Tana River. Ni kama kwenda Uropa au Zurich kwa ndege. Tulikuwa tunasafiri kwa gari. Namshukuru Spika pia na Karani wa Seneti kwa kuiwezesha Kamati hii kutembelea kaunti hizo. Tulipofika Tana River, hakukuwa na hoteli nzuri ya kulala. Mahali ambapo tulilala tulitimuliwa na panya. Hali ilikuwa ya kuhuzunisha. Sio jambo la kucheka."
}