GET /api/v0.1/hansard/entries/440537/?format=api
HTTP 200 OK
Allow: GET, PUT, PATCH, DELETE, HEAD, OPTIONS
Content-Type: application/json
Vary: Accept
{
"id": 440537,
"url": "https://info.mzalendo.com/api/v0.1/hansard/entries/440537/?format=api",
"text_counter": 194,
"type": "other",
"speaker_name": "",
"speaker_title": "",
"speaker": null,
"content": "Hata hivyo, Kamati iliendelea na kazi yake. Tulikutana na Gavana na mkuu wa elimu wa kaunti hiyo. Tuliwaeleza nia na madhumuni ya Kamati yetu, kwa sababu tulitaka kuona hali halisi ya shule za chekechea katika Tana River. Bw. Spika wa Muda, tulipotoka Tana River, tuliingia Kilifi. Unapoenda hosipitalini, kuna wodi tofauti. Kuna ICU ambacho ni chumba cha watu mahututi. Hii ndio hali ya Kaunti ya Kilifi ambayo inajumuisha Malindi. Hali ya elimu ya chekechea ilikuwa mbovu zaidi. Tulipotoka hapo, tulienda Mombasa ambayo ndio jiji. Kule hali ni afadhali kidogo. Wao hawakuwa ICU bali kwenye wodi. Bw. Spika wa Muda, tulipotoka hapo, tulienda kwa Kaunti ya Kwale, ambako mimi nawakilisha kama Seneta. Kule, hakuna hata vyoo vyaa kutumiwa na wanafunzi. Pia, hakuna maji. Ilikuwa hali ya kuhuzunisha na ndio maana tuliamua kuleta Ripoti hii ili ijadiliwe na kuchukuliwa hatua. Pia, tulizungumza na Magavana na tunawashukuru wote. Wengi wao walijitolea kukutana na kuongea nasi. Pia, walitupatia changamoto ambazo wako nazo. Pia, nasi kama Seneti, tuliwapa fikira zetu kuhusu jinsi ya kuzisaidia kaunti hizo. Bw. Spika wa Muda, changamoto moja ilikuwa inahusu shule za chekechea. Hakuna walimu wa kutosha wenye taaluma ya kufundisha wanafunzi ambao ni wachanga. Wale walimu walioko hawana taaluma hiyo. Pia, kuna uhaba wa vifaa vya kufunzia. Kati ya shule tulizozitembelea, tuliona kwamba wanafunzi wa Darasa la Kwanza wanatumia darasa ambalo linatumiwa pia na wanafunzi wa chekechea. Hii ni hali ngumu sana. Bw. Spika wa Muda, pia tulikuwa tumelitilia umuhimu sana swala la vyuo vya ufundi. Katika kaunti hizi, kuna vyuo ambavyo vilikuwa vinaitwa village polytechnics. Vyuo hivi vya ufundi vilikuwa na tatizo kubwa kupata wanafunzi kwa sababu hakuna mwanafunzi ambaye angependa kuhusishwa na kitu kinachoitwa “ Village Polytechnic”. Wengi walikuwa katika vyuo hivi vya ufundi, na sisi kama Kamati tukaonelea ya kwamba kuna haja ya vyuo vya ufundi hivi kubadilishwa majina badala ya kuitwa hivyo viwe vyuo vya ufundi ambavyo vitakuwa vinachukua wanafunzi kuanzia darasa la saba hadi la nne. Bw. Spika wa Muda, kuna msemo wa Kiswahili ambao unasema; “Kuvuta sana sio kulenga”. Hii tabia ya kuvuta sana halafu tunalenga kombo, haya ndio matatizo tulio nayo. Kila mahali kamati yetu ilipofika, Magavana walikuwa wazuri kwa kutueleza shida zao ambazo hazitatutliwi. Hakuna bajeti ya kufanya shughuli hii. Kama kuna bajeti, haina pesa za kutosha."
}