GET /api/v0.1/hansard/entries/440539/?format=api
HTTP 200 OK
Allow: GET, PUT, PATCH, DELETE, HEAD, OPTIONS
Content-Type: application/json
Vary: Accept
{
"id": 440539,
"url": "https://info.mzalendo.com/api/v0.1/hansard/entries/440539/?format=api",
"text_counter": 196,
"type": "other",
"speaker_name": "",
"speaker_title": "",
"speaker": null,
"content": "Kuna upungufu mkubwa katika bajeti. Na ndio maana tunasema ya kwamba hali hii itahitaji serikali zetu za kaunti ziongezewe hela za matumizi kwa sababu pesa ambayo Serikali kuu inapatia serikali za kaunti kwa kutekeleza majukumu zao hazitoshi. Ninamuona Sen. Murkomen akinitazama na mimi ningependa kumwambia kwamba huo ndio ukweli. Pesa hazitoshi katika serikali zetu za kaunti. Hizi shida ambazo tuko nazo si kwamba zilikuwa hazijulikani lakini kila mahali unapofika, lugha ni hiyo hiyo ilhali tulilianzisha serikali za ugatuzi kusudi kuhakikisha kwamba wananchi wetu wanapata manufaa. Ukweli ni kwamba baada ya miaka mitano, tutaenda mbele ya wananchi. Suti hizi na tai zenu zitakauka siku hiyo mkiulizwa na wananchi kile ambacho mmeleta. Huo ndio ukweli wa mambo, mimi nikiwa mmojawao, na Sen. Wamatangi na Sen. Murkomen. Ukweli ni kwamba wananchi wa Kenya hivi sasa wanataka kuona matokeo. Kule tulikotembelea, hali tuliyoiona siyo hali nzuri; ilikuwa ni hali ambayo haiwezi kutamanika miaka 50 baada ya Uhuru. Kwa hakika, ukitazama katika takwimu hizi, wilaya tano zinatoka katika Mkoa wa Pwani wa zamani. Ukitazama vile zinavyohitimu katika mitihani ya kitaifa, kama Lamu siyo ya mwisho, inafuatwa na Kwale, kama Kwale siyo ya mwisho inafuatwa na Kilifi. Sisi tunashika mkia kule nyuma. Hilo silo jambo la kufurahisha; hii ni hali duni na huo ndio ukweli. Ukitazama takwimu zilizotolewa na Waziri wa Elimu juzi, wanafunzi katika kaunti ya Kwale ama Kilifi wanaokwenda katika vyuo vikuu, Kwale ni 300, Kilifi, 400, Tana River, 78, Lamu, 90 na Nyeri, 4,000. Sasa watu 300 watawafikia watu 4,000 wakati gani? Kwa hivyo, ni lazima kaunti hizi zipewe mgao mkubwa wa fedha kusudi ziweze kuinua hali ya elimu.Tunasema tupeane mgao mkubwa kwa zile kaunti ambazo tunajua ziko hohehahe"
}