GET /api/v0.1/hansard/entries/440546/?format=api
HTTP 200 OK
Allow: GET, PUT, PATCH, DELETE, HEAD, OPTIONS
Content-Type: application/json
Vary: Accept

{
    "id": 440546,
    "url": "https://info.mzalendo.com/api/v0.1/hansard/entries/440546/?format=api",
    "text_counter": 203,
    "type": "other",
    "speaker_name": "",
    "speaker_title": "",
    "speaker": null,
    "content": "tulikuwa tunaelezwa kwamba Serikali inalipia baadhi ya wanafunzi, lakini ukitazama pesa hizo ambazo zinatoka kwa Serikali, kufika huko ilikuwa ni mtihani mwingine. Zilikuwa hazifiki kwa wakati unaofaa na kuathiri hali ya elimu. Mwenyekiti wa Kamati alitoa ushauri kwa watu wa pwani kwamba kwa sababu kuna uvuvi inafaa vyuo vya ufundi viwe vinafundisha watu masuala ya uvuvi. Kule Kwale, kuna madini na inafaa wanafunzi wawe na syllabus ya masuala ya madini. Tulikuwa tunapata syllabus inayofanana katika kila chuo cha ufundi; yale unayoweza kupata Nairobi na yale ambayo unapata katika kaunti zote ilhali haziendi sambamba na hali halisi ya kaunti hizo. Hii ilifanya masomo kuwa magumu sana. Kwa hivyo, kuna haja ya Kamati za Seneti kutembelea kaunti ili kujua hali ilivyo. Waswahili wanasema: “Anayekaa na mgonjwa ndiye anayejua hali ya mgonjwa”. Lakini wewe kila siku uko Kaunti ya Nairobi na unataka kuzungumza masuala yanayohusu Kaunti ya Tana River au Lamu. Utayajuaje? Ndio maana Mwenyekiti akaongoza ujumbe huu kwenda katika kaunti hizi. Hali tuliyoiona sio siri; hii ni hali ambayo hata kesho ukienda huko, hali hii iko vivyo hivyo. Ukiisoma Ripoti ya Kamati hii, utaona kwamba hatukwenda tu kutizama kwa macho, bali tulitoa mapendekezo kinaga ubaga kuhusu njia ya kufuata. Kwa kimombo inaitwa"
}