GET /api/v0.1/hansard/entries/440912/?format=api
HTTP 200 OK
Allow: GET, PUT, PATCH, DELETE, HEAD, OPTIONS
Content-Type: application/json
Vary: Accept

{
    "id": 440912,
    "url": "https://info.mzalendo.com/api/v0.1/hansard/entries/440912/?format=api",
    "text_counter": 314,
    "type": "speech",
    "speaker_name": "Hon. (Ms.) Chidzuga",
    "speaker_title": "",
    "speaker": {
        "id": 751,
        "legal_name": "Zainab Kalekye Chidzuga",
        "slug": "zainab-kalekye-chidzuga"
    },
    "content": "wachukuliwe na wapewe mafunzo zaidi ili waweze kusaidia jamii. Ni watu ambao wanaishi nasi katika jamii na wameweza kuokoa maisha licha ya kwamba hawajawahi kwenda shule. Lingine ni kwamba hili baraza linalonuiwa kuundwa, liwafikirie wale ambao hawakusomea hii taaluma shuleni ili nao wawakilishwe katika hilo baraza. Hii ni kwa sababu watu hawa wataleta maarifa wanayoyapata kule nyanjani. Wakenya wenzetu wanaosomea hii taaluma na kufanya kazi katika nchi za nje bado ni watu wetu. Tukifungua mlango ili waweze kurudi nyumbani na kufanya kazi humu nchini itakuwa ni bora kwetu. Tunapoteza pesa nyingi wakati hawa watu wanafanya kazi zao huko nchi za nje. Vile vile, tunapoteza pesa nyingi wakati tunawatuma wagonjwa wetu kwenda kupata matibabu nchi za nje. Hawa ambao wana ujuzi pia, Serikali iweze kufikiria kupanua zile hospitali ambazo tuko nazo ili wawahusishe. Waweze kupatiwa leseni na kuweza kuondolewa malipo ya KRA ili waweze kuleta mashine zao kutoka nchi za nje."
}