GET /api/v0.1/hansard/entries/441653/?format=api
HTTP 200 OK
Allow: GET, PUT, PATCH, DELETE, HEAD, OPTIONS
Content-Type: application/json
Vary: Accept
{
"id": 441653,
"url": "https://info.mzalendo.com/api/v0.1/hansard/entries/441653/?format=api",
"text_counter": 365,
"type": "speech",
"speaker_name": "Hon. Kombe",
"speaker_title": "",
"speaker": {
"id": 250,
"legal_name": "Harrison Garama Kombe",
"slug": "harrison-kombe"
},
"content": "tunaweza kujivunia kutokana na Kituo hicho. Wakaaji wa Magarini wamebaki maskini. Tunavyozungumza, barabara ya kwenda Ngomeni kutoka Mjanaheri haipitiki. Gari linalotembea kwenye barabara hiyo ni moja tu. Kituo kile kimekuwa pale kwa muda wa zaidi ya miaka 50 sasa, lakini hakuna chochote ambacho tunaweza kujivunia, kama wakaaji wa Magarini. Kenya imechelewa! Ingekuwa imechukua Kituo hicho punde tu makubaliano ama kadarasi ilipokwisha mara ya kwanza. Wakati huu tungekuwa mbali sana. Hivi ninavyozungumza, Serikali ya Italy inapata Kshs54 bilioni kila mwaka kutoka kwa Serikali ya Ufaransa peke yake, mbali na zile nchi zingine. Kiwango hicho kingesaidia Kenya kusonga mbele katika nyanja hii ya tekinologia ya angani. Hakika kwa wakati huu, hakuna haja hata kamwe kuwaruhusu Waitaliano kuendelea kutumia Kituo hicho. Hivi ninavyozungumza, inawapasa wahusika katika Serikali wachukue hatua kwa sababu kuna mipango ya kuyaahamisha mamlaka ya kituo hicho kutoka kwa makubaliano baina ya Kenya na Serikali ya Italy iwe kwa mabakubaliano baina ya Serikali ya Kenya and Chuo Kituu Cha Roma. Ikifanyika hivyo, tutakuwa katika hali ya kutofahamu. Hivyo basi, inafaa hatua ya dharura ichukuliwe na Serikali ya Kenya kuhakisha ya kwamba muda unapoisha mnamo tarehe 21 June, 2014, maneno hayo yawe yamekwisha. Hakuna tena kurudisha makubaliano baina ya Serikali ya Kenya na Serikali ya Italy. Wanasema kwamba wametoa Kshs240 milioni kusaidia ujenzi wa mahospitali, mashule na barabara katika sehemu tofauti. Jambo la kusikitisha ni kwamba katika kijiji cha Ngomeni, mahali ambapo Kituo hicho kipo, nyumba za wananchi zinaendelea kubomoka kama ilivyoonyeshwa katika runinga juzi. Wao wamejijengea ukuta mkubwa mahali ambapo hapaharibiki. Wale wenyeji, pale majirani, nyumba zao zinaendelea kuanguka. Katika mwaka wa 1975, kulikuwa na ofisi kubwa ya uvuvi. Kwa bahati mbaya hivi sasa, hiyo nyumba haiko. Imebomolewa na maji. Kulikuwa na hoteli kubwa hapo kando kando ya Ngomeni lakini hiyo pia imebomolewa. Kulikuwa na kituo cha askari wa majini hapo mbele ya San Marco Space, ambacho pia kimebebwa na maji. Hakuna msaada wowote ambao umepatikana kutoka kwa San Marco Space ilhali wanakusanya hela nyingi. Angalau wangeongezea ukuta wao ndani ya bahari na kwenda upande mwingine ili kuhifadhi zile nyumba na maeneo ya watu wengine; ingekuwa bora. Hivi sasa, maji ya bahari yanaingia mashambani na “kuua” mimea. Minazi “inakufa” kwa sababu ya maji ya bahari. Kule kwao wameyazuilia. Wameweka gome na hivi sasa, maji yanatiririka kwa mashamba. Wakati ni sasa kwa Serikali ya Kenya kukichukua Kituo hicho na kukimiliki kwa manufaa ya Wakenya. Kwa hayo machache au mengi, ahsante."
}