GET /api/v0.1/hansard/entries/442018/?format=api
HTTP 200 OK
Allow: GET, PUT, PATCH, DELETE, HEAD, OPTIONS
Content-Type: application/json
Vary: Accept
{
"id": 442018,
"url": "https://info.mzalendo.com/api/v0.1/hansard/entries/442018/?format=api",
"text_counter": 324,
"type": "speech",
"speaker_name": "Hon. Wario",
"speaker_title": "",
"speaker": {
"id": 252,
"legal_name": "Ali Wario",
"slug": "ali-wario"
},
"content": "Ninachukua fursa hii kumpongeza mhe. Mbadi kwa kuuleta Mswada huu Bungeni. Kwanza kabisa, ningependa kusema kwamba ninauunga mkono Mswada huu. Mimi ni Mbunge anayeegemea upande wa Serikali. Sitoshawishika kuunga mkono kupitishwa kwa sheria yoyote ambayo ni kinyume na Katiba ya nchi hii. Ninasema hivi kwa sababu nimebahatika kusoma kumbukumbu ya aliyekuwa Rais wa Zambia, mhe. Kenneth Kaunda. Mhe. Kaunda ni miongoni mwa viongozi ambao hawajawahi kufungua akaunti ya benki nje ya nchi zao. Alihudumia taifa lake na kuhakikisha kwamba ameliboresha. Alistaafu akiwa maskini. Sitofurahia leo kuwaona wale ambao walijitolea mhanga kuhakikisha kwamba taifa la Kenya limepiga hatua kwenda mbele wamerudi katika umaskini kufikia kiwango cha kutoweza kujitibu wanapoathirika na maradhi. Hii ndiyo sababu ninaiunga mkono Hoja hii. Pili, kuna neno moja nililolisoma katika Biblia. Nino hilo linasema kwamba wale wakwanza watakuwa wamwisho na wamwisho watakuwa wakwanza. Pengine tunafanya hivi kwa sababu tuko kwenye mrengo wa Serikali. Tutaweka vishawishi. Tutafunga barabara ili fulani na fulani asifaidi. Naomba tuangalie taifa na taasisi; tusiangalie watu. Ikiwa tutaangalia watu basi tutatunga sheria ambazo zitawatatiza watoto wetu siku za usoni. Ningependa kulinganisha wabunge wa hapa Kenya na wabunge kutoka nchi za nje. Tuchukulie mfano wa Afrika Kusini na tuseme kwamba familia ya Mandela imesemekana haitalipwa hela kwa sababu Mandela alihusika na kampeni za ANC. Ama tuchukulie mfano mwingine wa nchi jirani Tanzania na tuseme kwamba familia ya Mwalimu Kabarage Nyerere isilipwe malipo ya uzeeni kwa sababu alihusika kwenye kampeni za CCM. Kwa kweli haya mambo hayataingia akilini. Kipengele cha tatu katika Mswada huu kinakwaruzana na Kipengele 38(1). Mimi nitakuwa wa kwanza kuleta marekebisho ili kuhakikisha Kipengele hicho cha tatu kimetolewa. Hii ni kwa sababu ni sheria ambayo inadhulumu na inakwaruzana na Katiba ya nchi hii. Kwa nini tutunge sheria kama hizi? Naunga mkono Mswada huu. Ahsante, Bwana Naibu Spika wa Muda."
}