GET /api/v0.1/hansard/entries/442361/?format=api
HTTP 200 OK
Allow: GET, PUT, PATCH, DELETE, HEAD, OPTIONS
Content-Type: application/json
Vary: Accept
{
"id": 442361,
"url": "https://info.mzalendo.com/api/v0.1/hansard/entries/442361/?format=api",
"text_counter": 277,
"type": "speech",
"speaker_name": "Sen. Muthama",
"speaker_title": "",
"speaker": {
"id": 96,
"legal_name": "Johnson Nduya Muthama",
"slug": "johnson-muthama"
},
"content": "Bw. Spika, nilikuwa nikisema wananchi ambao waliathirika na wengine kuumia ni watu wetu na wanatusikiza sasa hivi. Wanataka kujua hasa, ni nini tunachosema kuhusu usalama wao. Ningependa kutuma ujumbe wa haki na ukweli. Jambo hili sio la chama fulani, kabila fulani ama kundi fulani. Vijana wetu wa kitengo cha ulinzi walikufa huko Baragoi. Hadi leo, hatujajua ni nini kilitendeka. Hapa Westgate, watu wetu walikufa, kule Mandera, watu wengi wamekufa. Nashangaa kwamba Seneta wa sehemu hiyo amesimama kukana kwamba AlShabaab hawahusiki. Tunajua vizuri kwamba hakuna mtu ambaye anaweza kutoka Mkoa wa Central, Eastern ama Coast na kusafiri hadi Mandera ili kuua Wakenya wenzake. Tunajua shida yetu ni nini. Mimi nilikuwa katika mstari wa mbele kusema kwamba hatufai kuyatoa majeshi yetu Somalia, tukae pale, tutafute adui na tumwangamize pale. Kulingana na vile usalama umezorota – huko Mpeketoni, kuna miili ya watu ambayo jamaa zao hawajui walichokosa. Kwa nini walikufa? Waliiba mali ya nani? Hawajui kufanya siasa. Waliamka siku moja, wakapiga kura na wakamaliza mambo hayo. Wale wanaohusika na ulinzi, tukianza na Rais mwenyewe, wanasema hiki sio kitendo cha maharamia bali ni kitendo kilichotokana na wanasiasa fulani. Rais hawezi kusema mambo hayo bila kupewa habari na watu ambao wanahusika na usalama. Hawa ndio humpa taarifa za ulinzi. Kama kitengo cha upelelezi kilijua mambo hayo, je, kilifanya nini? Ningependa ijulikane kwamba tunatafuta suluhu. Wenzangu, naomba kwamba mtakubaliana nami kuwa nchi yetu ina makabila 42. Mheshimiwa Spika, Katiba yetu, tuliyoipitisha sisi yasema kwa uwazi kwamba ni lazima izingatie jinsia na vile vile uwakilishi wa makabila yote katika Serikali. Kuna upungufu pahali fulani, kwa sababu ukiangalia kwa makini, yule Mkuu wa Majeshi katika taifa letu anajulikana ni nani na anatoka wapi, mkuu wa NIS anajulikana ni nani na anatoka wapi, mkuu wa kitengo cha upelelezi anajulikana ni nani na anatoka wapi, mkuu wa sheria ambaye anakaa katika Kamati ya Ulinzi anajulikana ni nani na anatoka wapi, Solicitor-General anajulikana ni nani na anatoka wapi, Katibu wa mambo ya usalama anajulikana ni nani na anatoka wapi---"
}