GET /api/v0.1/hansard/entries/442369/?format=api
HTTP 200 OK
Allow: GET, PUT, PATCH, DELETE, HEAD, OPTIONS
Content-Type: application/json
Vary: Accept
{
"id": 442369,
"url": "https://info.mzalendo.com/api/v0.1/hansard/entries/442369/?format=api",
"text_counter": 285,
"type": "speech",
"speaker_name": "Sen. Muthama",
"speaker_title": "",
"speaker": {
"id": 96,
"legal_name": "Johnson Nduya Muthama",
"slug": "johnson-muthama"
},
"content": "Asante, Bw. Spika. Tunataka kuona polisi wetu na kitengo cha upelelezi kikifanya kazi. Tunaweza kusema kwamba hiyo ndio sababu hawataki kufanya kazi yao kwa sababu hawajawakilishwa katika uongozi wa juu na maslahi yao hayaangaliwi sawa sawa. Kwa hivyo, tuliposema kwa Katiba kwamba tuwe na uwakilishi wa jinsia na makabila, haikumaanisha kwamba tuna ubaguzi wa ukabila. Tulisema kwamba kila sura iwakilishwe katika utumishi wa juu wa Serikali ndio wananchi waweze kufurahia nchi yao na kufanya kazi. Kwa hivyo, ninamwomba Rais aweke sura ya Kenya katika utumishi wa Serikali ili Wakenya wote wawakilishwe na ili taifa liwe na amani. Ninashukuru."
}