GET /api/v0.1/hansard/entries/442387/?format=api
HTTP 200 OK
Allow: GET, PUT, PATCH, DELETE, HEAD, OPTIONS
Content-Type: application/json
Vary: Accept
{
"id": 442387,
"url": "https://info.mzalendo.com/api/v0.1/hansard/entries/442387/?format=api",
"text_counter": 303,
"type": "speech",
"speaker_name": "Sen. Wangari",
"speaker_title": "",
"speaker": {
"id": 13123,
"legal_name": "Martha Wangari",
"slug": "martha-wangari"
},
"content": "Asante Bw. Spika kwa kunipa nafasi hii niweze kuchangia hii Hoja. Jambo la kwanza ni kutuma risala zangu za rambirambi kwa watu wa Mpeketoni na kwa Wakenya wote kwa jumla. Tarehe 15 Juni ni siku ya kimataifa ya kusherehekea akina baba ulimwenguni. Ningependa kusema kwamba wale ambao walikuwa na watoto wao wa kiume Mpeketoni na kula chakula cha jioni pamoja na asubuhi hawakuweza kuwaona tena. Naongea kwa uchungu, huzuni, masikitiko na hasira. Ninasema hivyo kwa sababu hakuna uhai ambao ni mkubwa kuliko wa mwingine; uwe ni wa mtoto kutoka Isinya, uwe ni wa mtoto kutoka Bungoma, West Pokot, Lamu, awe Mkikuyu or Masai, ni muhimu. Uwe ni uhai wa Sen. Wangari, Sen. Muthama au sisi sote, ni lazima ulindwe kwa vyo vyote vile. Uhai ni kitu cha maana sana. Uhai ni kitu kitakatifu. Tumefika mahali ambapo tunachukulia uhai kama kitu duni kabisa na ambacho hakina bei yoyote. Katiba yetu imelinda kabisa mambo ya uhai. Kuishi ni haki ya kila Mkenya. Bw. Naibu Spika, hatuwezi kuwa tunaongea kila siku hapa juu ya Wizara ya Usalama wa Ndani. Juzi tulishuhudia mauaji katika Kaunti za Samburu, Bungoma na kwingineko. Kila siku tunasema jambo moja. Ningependa kuunga mkono wale ambao wameongea kwa sababu hawa Wakenya ambao hawakupata nafasi ya kusherehekea kuitwa baba au kupikiwa na wake zao, hakuna yule ambaye ni muhimu kuliko mwingine. Kwa hivyo, hatuna budi kama Serikali kuweza kuleta mabadiliko katika Wizara ya Usalama. Bw. Spika, yale matamshi ambayo tunatamka kama viongozi ni lazima tuwe waangalifu kwa sababu yanaweza kusababisha maafa. Sitaki kusema mambo haya yalitokea kwa sababu ya kisiasa au yalisababishwa na magaidi. Ikiwa ni magaidi wa kutoka nje au majambazi wa humu nchini, ni lazima tufanye upelelezi. Hakuna vile watu 50 watafumania kijiji kimoja bila kuonekana. Halafu tunaambiwa kwamba walitokomea msituni au tunaambiwa kuwa ni mambo ya kisiasa. Akina mama wanalia kila siku. Nilikuwa nawatazama na kuwasikiliza kwa runinga. Hebu fikiria mama amewapoteza watoto wawili au mume wake. Hatuwezi kukaa hivyo na tuseme kwamba mambo haya ni ya kawaida."
}