GET /api/v0.1/hansard/entries/442503/?format=api
HTTP 200 OK
Allow: GET, PUT, PATCH, DELETE, HEAD, OPTIONS
Content-Type: application/json
Vary: Accept
{
"id": 442503,
"url": "https://info.mzalendo.com/api/v0.1/hansard/entries/442503/?format=api",
"text_counter": 419,
"type": "speech",
"speaker_name": "Sen. Madzayo",
"speaker_title": "",
"speaker": {
"id": 679,
"legal_name": "Stewart Mwachiru Shadrack Madzayo",
"slug": "stewart-mwachiru-shadrack-madzayo"
},
"content": "Bw. Naibu Spika, kwa niaba ya watu wa Kilifi, Pwani na Kenya kwa jumla, ningependa kutoa rambirambi zangu kwa wananchi wa Lamu waliopatikana na mkasa huu, hasa wale wa Mpeketoni na vitongoji vyake. Bw. Naibu Spika, ningependa vilevile kukubaliana na wale wenzangu waliotangulia kusema ya kwamba wale ambao wamezembea kazini, hasa kwa upande wa ulinzi waachishwe kazi mara moja. Maisha ya Mkenya akiwa Lamu, Kisumu, Mombasa, Kilifi au sehemu yoyote ya Kenya ni muhimu sana katika nchi hii. Leo itakuwa ni aibu tukisimama na kujidai kama Wakenya ilhali ndugu zetu wanaweza kupoteza maisha kirahisi na kiholelaholela. Vifo hivi vinavyotokea mahali popote katika Kenya yetu, vina athiri uchumi wetu. Hasa mimi natoka upande wa Pwani na mambo mengi yamefanyika huko. Mambo mengi yamefanyika Mombasa, Tana River na sasa katika Kaunti ya Lamu. Mambo haya yataathiri utalii wetu. Je, tunazingatia kwamba wale vijana waliofika umri wa kufanya kazi hivi sasa wameachishwa kazi katika sekta hii ya utalii. Wakulima wanaofuga kuku hawana mahali pa kuuza kuku na mayai yake. Pia wakulima The electronic version of the Senate Hansard Report is for information purposes only. A certified version of this Report can be obtained from the Hansard Editor, Senate."
}