GET /api/v0.1/hansard/entries/442505/?format=api
HTTP 200 OK
Allow: GET, PUT, PATCH, DELETE, HEAD, OPTIONS
Content-Type: application/json
Vary: Accept

{
    "id": 442505,
    "url": "https://info.mzalendo.com/api/v0.1/hansard/entries/442505/?format=api",
    "text_counter": 421,
    "type": "other",
    "speaker_name": "",
    "speaker_title": "",
    "speaker": null,
    "content": "wanaopanda mboga, nyanya, matunda na kadhalika wameathirika sana. Je, watu hawa tunawafikiria vipi? Ikiwa sisi tunaweza kukaa hapa na kusema hakuna jambo lilotokea, tutakuwa tunafanya makosa makubwa. Bw. Naibu Spika, Wakenya walipiga kura na kumchagua Rais Uhuru Kenyatta. Tulikubaliana sote kuwa yule aliyechaguliwa na Wakenya kama Rais atatawala Kenya kwa kipindi cha miaka mitano. Huyu si mwengine, bali ni Rais Uhuru Kenyatta. Huyo ndiye Rais wa Jamhuri ya Kenya. Tulale leo, tuamke kesho; atoke aende ulaya arudi, akienda wapi na hata akiwa wapi, yeye ni Rais wa Jamhuri yetu ya Kenya. Hiyo inatambulika ulimwengu kote. Jambo la kusikitisha ni kwamba wale watu aliowaandika kazi, hasa katika idara ya ulinzi, hawaonekani kuwa makini kwa kazi yao. Tunaambiwa kwamba wahalifu waliingia Mpeketoni saa 2.00 za usiku na wakaanza vita. Simu zikapigwa lakini usaidizi haukuja hadi baada ya masaa saba. Hii ni kusema kwamba ni ukweli kuna watu waliozembea kazini. Ikiwa inaweza kuchukua masaa saba kufika Lamu, ilhali tunaona wakati wa sherehe ya Madaraka, ndege za kivita zinapita hapa mbio kama umeme, ni sababu gani ilikuwa hatuwezi kutuma hata watu wetu walioko Malindi wakimbie pale kusaidia? Wao wangechukuwa saa moja tu. Kwa hivyo, kufikia saa tano wangefika pale na kuwasaidia wale Wakenya walioko pale na kuokoa maisha yao. Kwa nini walichukua masaa saba? Hilo ndilo swali Wakenya lazima wajiulize na wajibiwe. Bw. Naibu Spika, kwa hayo machache, ninaomba kuunga mkono hoja hii."
}