GET /api/v0.1/hansard/entries/442615/?format=api
HTTP 200 OK
Allow: GET, PUT, PATCH, DELETE, HEAD, OPTIONS
Content-Type: application/json
Vary: Accept
{
"id": 442615,
"url": "https://info.mzalendo.com/api/v0.1/hansard/entries/442615/?format=api",
"text_counter": 109,
"type": "speech",
"speaker_name": "Sen. (Dr.) Machage",
"speaker_title": "",
"speaker": {
"id": 179,
"legal_name": "Wilfred Gisuka Machage",
"slug": "wilfred-machage"
},
"content": "Bw. Spika, kwa niaba yangu mwenyewe na wananchi wa Migori County, ninatuma rambirambi zetu kwa familia na marafiki wa huyu Gen. Mulinge ambaye alikuwa mcheshi, mzalendo na aliyependwa na watu nchini. Kazi yake ilidhihirika na uwezo wake ulionekana kwa kazi aliyopewa. Si wengi wetu walio kama yeye alivyokuwa wakati wa uhai wake. Lakini pia tunamshukuru Mungu kwamba aliishi miaka mingi. Umri wake si jambo la kawaida kwa wengi nchini. Hata kama tunalia na kutoa machozi, pia ni lazima tusherehekee maisha marefu aliyopewa na Mwenyezi Mungu huyo mzalendo wa nchi ya Kenya. Tukubali yaliyotendeka na kumshukuru Mungu kwa maisha yake. Asante, Bw. Spika."
}