GET /api/v0.1/hansard/entries/442875/?format=api
HTTP 200 OK
Allow: GET, PUT, PATCH, DELETE, HEAD, OPTIONS
Content-Type: application/json
Vary: Accept

{
    "id": 442875,
    "url": "https://info.mzalendo.com/api/v0.1/hansard/entries/442875/?format=api",
    "text_counter": 145,
    "type": "speech",
    "speaker_name": "Sen. (Dr.) Machage",
    "speaker_title": "",
    "speaker": {
        "id": 179,
        "legal_name": "Wilfred Gisuka Machage",
        "slug": "wilfred-machage"
    },
    "content": "Asante sana, Bw. Naibu Spika. Niruhusu niseme yangu machache juu ya janga hili la kukosa usalama nchini. Tunapoongea jambo hili, tujue kwamba kwa kawaida, matibabu ya ugonjwa sio lazima kugonga pale uchungu ama maumivu yalipo; eti ukiumwa na kichwa, unaenda kukata kichwa kwa sababu uchungu uko kwa kichwa. Labda shida ni nyingine. Labda una viini au damu inakimbia sana. Kwa hivyo, ni lazima utafute ni sababu gani kichwa kinauma wala sio kukimbilia kukata kichwa. Hivyo ndivyo wenzetu labda wanafikiria juu ya jambo hili la usalama; kwamba labda kwa sababu kuna vita au watu wameuwawa sehemu fulani, inafaa Mkuu wa Polisi akimbie huko. Ni kwa nini watu wamekosa uzalendo? Ni kwa nini kuna kulalamika hata ikaja ikatokea vifo vya wananchi wa Kenya? Haya ndio mambo ambayo yanastahili kufikiriwa na tuyaongee kinaga ubaga kwa sababu si vizuri kuficha. Umaskini ndicho chanzo kikubwa cha wizi wa mifugo hapa na pale; kutokupata haki inayotosha, inayoonekana kwamba inalingana kwa binadamu wa nchi hii wote. Kuna umuhimu wa kupeleka rasilmali iliyo sawa vijijini nchini kote. Kukosa mawasiliano mazuri pia ni changamoto kubwa kwa sababu sehemu zingine hakuna barabara na viwanja vya ndege. Kwa hivyo wezi wanapata nafasi ya kufanya yale wanaoyofanya wakijua kwamba Serikali haitawafikia haraka. Kuna changamoto ya siasa. Wengine hawakukubali kwamba labda uchaguzi ulitendwa kwa haki. Wamekosa vile watakavyosema, na kwa hivyo wanaona ni lazima wachukue silaha na kuanza kupigana, na kadhalika. Kwa hivyo, ni lazima tuangaze mawazo yetu kwa fikra ambazo zina maana kwa mambo ya usalama nchini. Lakini hata hivyo, ni kufundisha wananchi kwamba wao wenyewe; watu 42 milioni, wana jukumu; kila mtu kibinafsi kuchukua usalama wa nchi yao kama jambo la uzalendo. Kwa sasa hivi, maofisa wa Serikali na polisi ambao tuko nao hawawezi kuhudumia kila mtu kwa sababu ni mmoja kwa watu 4,000. Haiwezekani kila mtu kuwa The electronic version of the Senate Hansard Report is for information purposes only. A certified version of this Report can be obtained from the Hansard Editor, Senate."
}